Monday, July 28, 2008

Benki ya Dunia Wailipe Fidia Serikali
-Mkono
Wakili Nimrod Mkono(Kulia)akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari Ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
--------
Wakili maarufu nchini,Nimrod Mkono aliyekuwa akiitetea Serikali ya Tanzania dhidi ya kampuni mama ya City Water ya BiWater Gauff Tanzania Limited(BGT)na kushinda katika kesi mbili, amesema Benki ya Dunia ndiyo ingepaswa kuilipa fidia Tanzania kwa kuishawishi kuingia mkataba na kampuni hiyo ya huduma ya maji.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya ushindi huo wa Serikali ya Tanzania,Mkono ambaye ni Mbunge wa Musoma Vijijini,alisema Benki ya Dunia ndiyo waliopitisha jina la BiWater kuja nchini kuboresha huduma ya maji.“Wao(Benki ya Dunia)ndiyo waliotaka tuwape kazi BiWater,lakini wao hawakuja bali waliungana na Gauff ya Ujerumani na kuundwa Kampuni ya BiWater Gauff Tanzania Ltd ambao waliunda City Water iliyoshindwa kazi,”alisema Mkono.Kwa Habari hii zaidi Bofya na Endelea.....>>>>

No comments: