Saturday, June 28, 2008

tigo yafanya kweli sabasaba 2008

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Biashara ya nje inayoandaa Maonyesho ya Biashara ya SabaSaba Mh. Ramadhani Khalfan akikata utepe lango kuu katika uwanja wa mwalim J K Nyere mara baada ya kampuni ya simu ya Tigo kukabidhi maeneo ya kimvuli cha kudumu yaliyojengwa na Tigo kwa ajili ya kuwakinga jua na mvua waalikwa na wageni watakaotembea viwanjani hapo wakati wa maonyeso kuanzia Jumamosi hii. Shoto ni bosi wa Masoko wa Tigo Kelvin Twissa.



Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya 32 ya sabasaba Julai 1, 2008, ambapo kutakuwa na maonesho ya nchi 27, wizara 9, idara 38 na serikali, kampuni za bongo 650 pamoja na wadau wa biashara ndogondogo 60, wakiwamo machinga ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Daily News na HabariLeo nao watakuwepo kufanya kile walichofanya wakati wa mkutano wa Sullivan A-taun kwa maonesho ya mapicha na shughuli za gazeti hilo mama la magazeti nchini ambalo limeendeleza libeneke kwa miaka 75 sasa.

Tigo ndio kampuni rasmi ya mawasiliano katika maonesho haya na tayari imeanda shughuli kibao na zawadi kedekede kwenye banda lake

No comments: