Tuesday, June 17, 2008

Mkutano wa Watanzania
Tokyo..


Mkuu wangu Kdidi,
Kama kawa salamu nyingi kutoka huku Mashariki ya Mbali.Mkuu wangu nitashukuru kama utapata nafasi kwenye blog yetu tukufu ukiweka baadhi ya picha zinazoonyesha mkutano wa Watanzania Wanaoishi Tokyo na miji ya jirani uliofanyika Odakyu Sagamihara siku ya Jumapili.Mkutano huo wa Watanzania wote uliitishwa kujadili masuala mbalimbali muhimu kuhusiana na jumuiya ya Watanzania hapa Japani.

Mkutano huo ulikuwa chini ya Balozi Mtango na ulihudhuriwa na karibu Watanzania 70. Maamuzi ya msingi yaliyofikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa Watanzania wote utakaochagua safu mpya ya viongozi wa kudumu wa Umoja wa Watanzania. Kamati husika imepewa kipindi cha mwezi mmoja kuhakikisha inafanikisha hilo.Shukrani mkuu wangu.

No comments: