Monday, June 30, 2008

Naibu Meya Dar atangaza
kujiuzulu...


Meya wa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam, Bw.Mohamed Yakubu (Pichani),ametangaza kujiuzulu nafasi aliyonayo kwa madai kuwa anataka kuachia wengine washike nafasi hiyo na yeye kuelekeza nguvu zake katika kujiendeleza kielimu. Taarifa za kujiuzulu kwa Bw.Yakubu zililifikia Majira Jumapili Dar es Salaam jana kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho kieleza sababu za kujiuzulu kwake.


Taarifa za kujiuzulu kwa Bw.Yakubu zililifikia Majira Jumapili Dar es Salaam jana kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho kieleza sababu za kujiuzulu kwake. Akizungumza kwa njia ya simu jana Bw.Yakubu alisema ni kweli yupo katika harakati za kujiuzulu nafasi ya Unaibu Meya wa Manispaa hiyo ingawa bado hajaandika barua rasmi kwa uongozi wake wa juu."Bado sijaandika baarua rasmi ya kujiuzulu nafasi hiyo lakini natarajia kuandika barua siku yoyote kuanzia kesho kuujulisha uongozi wangu wa juu akiwemo Meya wa Manispaa ya Ilala Alhaj Abuu Jumaa," alisema Bw.Yakubu.

Alisema kujiuzulu ni uamuzi mzito lakini kwa upande wake ameamua kufanya hivyo kwakuwa anatarajia kuanza masomo ya Utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani. Alisema pindi atakapoanza masomo yake itakuwa vigumu kwake kujihusisha moja kwa moja kutoa huduma kwa wananchi akiwa katika nafasi ya Naibu Meya.Habari na Na Said Mwishehe

No comments: