Friday, June 27, 2008

Mashindano Ya Karate..
Klabu ya Scorpion Shotokan karate-Do (Scoshoka) ya jijini Dar-es-salaam itafanya mashindano makubwa ya wazi ya mchezo wa karate mnamo Juni 28, 2008 (Jumamosi) katika ukumbi wa Don-Bosco Upanga jijini Dar-es-Salaam, mashindano hayo yanajulikana kama "JKA INDIVIDUAL OPEN TOURNAMENT 2008" yakiwa nalengo la kuhamasisha mchezo huokwa jamii, kupanua wigo wa ushirikiano na kuwahamasisha Watanzania washiriki kwani ni kama michezo mingine yoyote.

Haya ni mashindano ya pili, mara ya kwanza yalifanyika Juni 30, 2007 kwa mafanikio makubwa ambapo yaliwashirikisha makarate-ka zaidi ya 50 kutoka klabu za jijini Dar-es-Salaam. lakini mwaka huu yameboreshwa ili kuleta msisimko zaidi ambapo yatashirikisha klabu za jijini Dar-es-Salaam na kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Zanzibar, Iringa , Pwani na Morogoro. Tunatarajia makarateka zaidi ya 100 kushiriki.

Kikubwa zaidi mwaka huu ni kwamba, mashindano haya yatashuhudiwa na Mwakilishi wa Japan Karate Association (JKA) Kanda Afrika, Sensei Mtshali ( 7th Dan - Nanadan) kutoka Afrika Kusini. Ujio wake nchini ni muhimu sana kwa ustawi wa mchezo wa karate, kwani tunaamini kwamba Tanzania itakuwa imepiga hatua kwenye ramani ya mchezo huu duniani baada ya mashindano haya.

Mbali na Sensei Mtshali, pia kutakuwa na waamuzi watatu toka Kenya ambao ni Sensei David Murwa ambaye ni Mwenyekiti wa JKA-Kenya, Sensei Peter Ombima na Sensei Peter Njagi ambao watashirikiana na waamuzi toka Tanzania Sensei Yahya Mgeni, Sempai Caessar Mwansasu, Sempai Amos Lombo, Dadus na Gladys Obwaya.

Pia Kutakuwa na vingilio, ambapo Washiriki watalipia 3,000/= kila mmoja na Mtazamaji 5,000/=
Watanzania tufike na Wageni, tufike kwa wingi kushiriki na Kushuhudia Mashindano haya ya kusismua.
Nestory Fedeliko
Katibu - Scoshoka

No comments: