Monday, June 30, 2008

Chacha Wangwe asimamishwa
Chadema

KAMATI Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),imemsimamisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Chacha Wangwe (Pichani)kuendelea na wadhifa huo.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata zinaeleza kuwa,uamuzi wa kumsimamisha Wangwe ulifikiwa katika kikao cha siri cha Kamati Kuu kilichofanyika jana mjini Dodoma.
Kiongozi mmoja wa CHADEMA aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, alieleza kuwa uamuzi wa kumsimamisha Wangwe ulifikiwa kwa kauli moja na wajumbe wate wa Kamati Kuu isipokuwa Wangwe ambaye aliupinga.
Alisema, Wangwe amesimamishwa baada ya kubainika kuwa na makosa ya kukigawa chama katika makundi na kusababisha kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa katika ofisi za makao makuu.
Habari zaidi zilieleza kuwa,Wangwe amepinga uamuzi huo na anatarajiwa kuanza ziara ya mikoani yenye lengo la kuwaeleza wanachama kilichasababisha kufikiwa kwa hali hiyo.kwa mengi zaidi bofya Hapa

No comments: