Monday, June 30, 2008

Tanzanite Fc,Atlanta wajitolea kulipa
Jezi ya Mchezaji wa
Taifa Stars..
--------------------
Habari yako,
pole na shughuli nzito ya kuwakilisha jamii.Sisi Vijana wa Tanzanite fc Ya Atlanta Ga tunasikitika na habari tuliyosoma juu ya mchezaji wetu aliyewakilisha timu yetu ya taifa huko Cameroon kwa kuadhibiwa kwa kulipia jezi ya timu ya taifa aliyobadilishana na mchezaji mwenzie wa Cameroon(Etoo)tumeona kwamba ni swala la aibu kwa chama cha soka cha Tanzania kumdai mchezeji huyo hasa ukizingitia mchango wake kwa Taifa.
Sisi Tanzanite fc tungependa kujitolea kulipa deni hilo la huyo mchezaji. Je ni utaratibu gani tuutumie kuwakilisha mchango huo, na je ni kiasi gani?Tunatanguliza shukrani zetu kwa msaada wako kutufanikishia swala hili.
Wako
Tanzanite fcAtlanta,GA.
USA

No comments: