Tuesday, June 17, 2008

Kelly Rowland Kutua Bongo
jun 16..
MWANAMUZIKI nyota wa R&B, Kelly Rowland (pichani)anatarajia kutua Dar es Salaam Juni 16 majira ya mchana akitokea Afrika Kusini.Kelly,ambaye ni nyota wa lililokuwa kundi maarufu la Destiny Child lililowahi kutamba katika muziki duniani, ni balozi wa taasisi ya MTV Staying Alive Foundation ana anafika nchini ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika nchi kadha za Afrika.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania, Lucy Kihwele alisema akiwa hapa nchini anatarajia ,nyota huyo anatarajia kutembelea vituo kadhaa vinavyopambana na ugonjwa wa Ukimwi na kuzungumza na waandishi wa habari.Nyota huyo anaendeleza malengo ya taasisi ya MTV Staying Alive Foundation ya kuwawezesha vijana walio tayari kujikinga wenyewe na jamii yao na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kuwa na nafasi hiyo.Kihwele alisema baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini, Kelly anatarajia kwenda Kenya. Pia atatembelea nchi za Ghana, Msumbiji na Angola.

No comments: