Tuesday, December 28, 2010

WANANCHI AUSTRALIA WAKIMBIA MAFURIKO KATIKA JIMBO LA QUEENSLAND…!!!

Baadhi ya nyumba zilizokumbwa na mafuriko hayo


Mafuriko makubwa yaliyolikumba eneo la kaskazini –mashariki ya Australia yamewalazimisha maelfu ya wakazi wa maeneo hayo kukimbia huku yakiharibu barabara zaidi ya mia tatu (300).

Mafuriko hayo pia yamesababisha hasara ya mamilioni ya dola katika mashamba ya mazao ya alizeti na pamba.

Kufuatia siku kadhaa za kunyesha mvua mfululizo serikali katika jimbo la Queensland imetangaza maeneo kadhaa kuwa ukanda wa janga.

Hii inakuwa ni desemba ya kwanza kuwa na mvua kubwa na kusababisha mafuriko katika mji mkuu wa jimbo hilo Brisbane kwa kipindi cha zaidi ya miaka 150.

Miji ya ndani ya Theodore, Chinchilla na Dalby imefunikwa na maji, huku mji jirani wa Warra, na miji ya Alpha na Jericho magharibi mwa Emerald, pia imetangazwa kuwa maeneo ya janga

No comments: