Tuesday, December 28, 2010

Bagamoyo panazidi kupendeza.
Boma la Bagamoyo likipigwa sop-sop ili liwe kama mengine kibao yaliyokarabatiwa ama yanayokarabatiwa sasa na kuufanya mji huu mkongwe uwakewake na uzidi kuvutia watalii wa nje na wa ndani
mojawapo ya majengo yaliyokarabatiwa pamoja na barabara ambayo imejengwa kama iliyokuwa enzi hizo, sio kwa lami bali vitofali
Jengo lingine ambalo sasa linawaka ile mbaya baada ya
ukarabati na barabara mpya mbele yake

Hii ndiyo posta ya kwanza Afrika Mashariki karibu na bandari ya Bagamoyo. Hivi sasa inakarabatiwa na kuwa sehemu ya hoteli ya Millenium inayomalizia jengo lake kuu linaloangalia bahari kwa nyuma ya hii posta
Jengo jipya la Millenium bega kwa bega na posta ya zamani

No comments: