Saturday, December 25, 2010

Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha(kushoto)akipewa maelezo na maofisa wa Magereza, namna mfumo wa Teknohama katika jeshi hilo unavyofanya kazi.
----
Na Selemani Nzaro
JESHI la Magereza katika Mkoa wa Dar es Salaam limeingia katika mfumo mpya wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) katika uhalifu kwa Jeshi la Magereza.

Mfumo huo uliozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita utawezesha maofisa Magereza wakiwa makao makuu kupata taarifa za uhalifu wa wafungwa wakiwa magerezani, ambapo ofisa atafuatilia rekodi zinazoweka pasipo ulazima wa kusafiri.


Mfumo huo wa kisasa kabisa utaliwezesha Jeshi la Magereza kuweka taarifa za wahalifu yaani wafungwa na mahabusu katika mfumo huo hali itakayorahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu katika makao makuu.


Mfumo huo utahusisha wahalifu kutoka katika magereza matatu ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam. Taarifa za wahalifu kutoka katika magereza matatu ndani ya mkoa huo zitapatikana makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo katikati ya jiji.


Hii ina maana kama taarifa za mhalifu zimesahaulika askari hatalazimika kusafiri hadi katika gereza husika ili kupata taarifa hizo. Magereza yatakayohusika katika mpango huu ni yale ya Ukonga, Keko na Segerea.


Kukamilika kwa mradi huu wa Teknohama kunahitimisha safari ndefu ya kuuandaa iliyoanza mwaka 2000. Mwaka huo Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ilianzisha mradi uliokwenda kwa jina la ‘Kuimarisha Uwezo ili Kuboresha

Hadhi ya Haki za Binadamu Tanzania’.

No comments: