Tuesday, December 28, 2010

AU YAMTAKA RAILA KUSULUHISHA MGOGORO WA IVORY COAST…!!!

Bw.Raila Odinga


Umoja wa Afrika AU umemtaka Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kuongoza juhudi za umoja huo katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa unaofukuta nchini Ivory Coast ambako marais wawili tayari wameapishwa.

Juhudi hizo za kutafuta muafaka nchini Ivory Coast pia zinahusisha wakuu watatu wa mataifa ya Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Jean Ping amesema amemuomba Bw. Odinga kufuatilia hali ilivyo nchini humo na kuimarisha juhudi zinazochukuliwa kumaliza machafuko.

Akizungumza na vyombo vya habari, Bw. Odinga ametangaza kukubali jukumu alilopewa na Umoja wa Afrika AU, na kuahidi kuwa katika mgogoro huo hatafungamana na upande wowote ili aweze kuleta amani na maridhiano nchini Ivory Coast.

Aidha Bw. Raila ameongeza kusema kuwa Gbagbo anapaswa kupewa uhakika kuwa hakuna hatua mbaya zitakazochukuliwa dhidi yake kwani naye amekuwa akipigania demokrasi nchini humo.

No comments: