Saturday, December 18, 2010

BREKING NYUUUUZZZZZ: ABOU SEMHANDO WA TWANGA PEPETA AFARIKI AJALINI DAR
Marehemu Abou Semhando 'Baba Diana' enzi za uhai wake. Hapo ilikuwa katika show ya Old Skul viwanja vya Karimjee ambapo wakongwe wa muziki walikusanyika kutumbuiza
Marehemu Abou Semhando (kulia, fulana nyekundu) akiwa katika mazishi ya Dk. Remmy Ongala na wakongwe wenzie. Toka shoto ni Mzee Makassy, Tschinga Kalala Assosa, King Kikii na Kanku Kelly
Pikipiki ya Marehemu Abou Semhando baada ya kupata ajali
Gari linalosadikiwa kuhusika na ajali hiyo likiwa mtaroni

Na John Kitime

Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.

Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.


Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.


Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake.

No comments: