BREAKING NYUUUZZZZ:
CHENGE AFANIKIWA KUKWEPA LUPANGO
KWAKUTOA FAINI YA LAKI 7 LEO
Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania ikiwamo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, leo alipona kutupwa jela miaka mitatu baada ya kulipa faini ya sh 700,000 katika kesi yake kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.
Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo.
Rusema alisema kutokana na ushahidi wa watu sita uliotolewa,mahakamani imemhuona na hatia ya makosa manne ambapo alimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh 700,000.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rusema alisema kuwa,Mahakama imemkuta na katika makosa yote manne na kwa kosa la kwanza na la pili alitakiwa alipe faini ya sh 250,000 kwa kila kosa ambayo ni sawa na sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili na katika shitaka la tatu na la nne alitakiwa kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela mwaka mmoja.
Chenge alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake waWili,uharibifu wa mali na kuendesha gari bila kuwa na bima.