Monday, April 20, 2009

libeneke la ubabe wa manjagu
Habari Brother Kadidi.
Mimi ni mmoja wa wadau wa Blog yako. Haipiti Asubuhi bila ya kufungua na kuona nini kimejiri. Pia hutembelea sites/blog nyengine kwa lengo la kujihabarisha.
Leo katika Website ya BBC, nimepata hii (attachement), naomba sana uwarushie wadau wengine. Ukiweza, nifikishie salamu kwa Jeshi la Polisi Tanzania. Wao wanafanya jitihada gani kuzuia Unyanyasaji wa Raia kutoka Polisi?? (Juzi tuu, pale Buguruni nimemuona Askari wa Trafic anampiga Vibao Dereva wa DalaDala), Ni kweli alifanya Uzembe, lakini jee hii ndio sheria??
Mimi ni mmoja ya watu wanaokerwa sana na vitendo viovu vya Polisi Watanzania. "Unyanyasaji, Rushwa na kutokujali sheria za Nchi" Kwa bahati mbaya hapa Tanzania, hakuna mtu anaewakemea. Hivi ni kweli kazi yao haina Maadili?.
Ok, hii imetokea Uingereza na bado mziki unaendelea. Habari kamili
Mdau Salim,
Kitunda.

No comments: