Saturday, April 25, 2009

libeneke la muungano na uraia wa nchi mbili
Mzee Nelson Madiba MANDELA anaichoma moto PASSPORT ya KIKABURU ya Afrika Kusini,na anabaki kuwa raia wa asili wa AZANIA yaani Afrika Kusini)
Kuwa na Pasi ya US,Ulaya,uhajemi nk.akumfanyi mtanzania kubadilika heti hasiwe mtanzania au mswahili tufungue macho

Sherehe za Muhungano Zinanukia! Na Uraia wa nchi mbili nao?

Sherehe za kumbu kumbu ya sikuu ya muhungani zinanukia kwa kila mtanzania aliye nje au ndani ya nchi,ni sikukuu ya kumbu kumbu ya kitendo cha kihistoria kilichotuhunganisha watanganyika na wazanzibar ikazaliwa Tanzania nasi tukaitwa watanzania jina au uraia ambao ukienda popote duniani na kujitambulisha hivyo basi utapata heshima ya hali ya juu! kuwa umetoka katika nchi ya waungwana wasio kubali kutawaliwa! pia kugawanywa.

Historia hii inawasuta walio wengi aswa mataifa ya ulaya ya magharibi ambao walijua kuw amuhungano huu hauwezi kudumu!

LAKINI TUJIULIZE SWALI MOJA ? JE PAMOJA NA MATUNDA MENGI YA MAFANIKIO YA MUHUNGANO ? VIPI KIUCHUMI? TUPO UHURU? YAANI SIO TEGEMEZI?TUFANYE NINI? HILI TUSIWE TEGEMEZI LA KUTEGEMEA MISAADA SANA?

Hapa ndipo tuanzie kuzungumuzia swala la URAIA WA NCHI MBILI ambao unataweza kumuruhusu mtanzania kuwa raia wa nchi nyingine bila ya kupoteza uraia wake wa hasili wa tanzania ambao ni wa jamuhuri ya muhungano! kama uwezekano huo hupo basi utakuwa kwa faida ya Tanzania kutumia watanzania wachache walio nje ya nchi kuleta maslahi nyumbani Tanzania kwa faida ya taifa pia kwa familia zao.

Swala hili la urai wa nchi mbili atuwezi kulikwepa na kwa kadri linavyopigiwa MIZENGWE!

ndivyo tutakavyo kuwa nyuma na matokeo ya watanzania tutajikuta tunafungwa bao la kisigino na majirani zetu waliotunguzunguka!!!! kwani nao kwa namna moja au nyingine tumeungana nao japokuwa si kwa jina la JAMUHURI YA MUHUNGANO bali kwa jina la
JUMUHIYA YA AFRIKA MASHARIKI hata pia Kwa muhungano wa jina la SADIC n.k
Wenzetu hao washaanza kula matunda ya uraia wa nchi mbili na kuhakikisha kila manufaa wanapeleka kwao kutoka ughaibuni! wakati watanzania bado tunaliweka swala hili katika mambo ya kisiasa!
Hivi tunachokiogopa ni nini ?aswa katika swala zima la uraia wa nchi mbili?na kulifanya swala zima liwe la mizengwe,na penginepo baadhi ya vyama vya kisiasa watalichukulia ndio MADA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI!
Hivi watoto wangapi waliozaliwa nje au ndani ya Tanzania ambao moja ya wazazi wao ni mtanzania !au pengine wazazi wao wote ni watanzania lakini watoto hao kwa kuwa wazazi wao hawana uraia wa nchi mbili kunawafanya watoto hao kukosa uduma fulani muhimu?
Tuchukulie labda wazazi wa mtoto wanaishi ulaya,marekani,Asia,Uhajemi na kungineko!
na mtoto kazaliwa huko ughaibuni na sheria ya huko inasema kama mtoto sio raia wa kujiandikisha awezi kupata uduma za bure za matibabu ya nchi hiyo?itabidi wazazi walipe gharama kubwa kwa kutibiwa mtoto wao kisa mtoto ana uraia wa nchi mbili!
Au mtoto itabidi alipiwe ada ya bei ya juu ya masomo kwa kuwa si raia wa nchi mbilijapokuwa kazaliwa huko ughaibuni na anayo haki ya kuwa raia wa huko! lakini sheria ya jamuhuri ya muhungano haimruhusu! je nani ni mwenye hasara?
Mwisho kabisa ninawatakieni heri ya siku kuu ya mhungano na pia tujaribu kuweka AGANO JIPYA KATIKA MUHUNGANO WETU!

NA AGANO HILO NI KULITUPIA JICHO SWALA LA URAIA WA NCHI MBILI NA KWA FAIDA YA NANI?

Mdau Msemakweli

No comments: