Saturday, April 25, 2009

ajali kilosa
Mh. Profesa Mark Mwandosya (shati jeupe) akipiga simu kuomba msaada muda mfupi baada ya ajali kutokea. Mbunge wa zamani wa Biharamulo Magharibi ndugu FAUSTINE KABUYE alifariki katika ajali hiyo pamoja na watu wengine wawili sehemu za Kilosa mkoani Morogoro iliyohusisha basi la RS investment likitokea Bukoba kwenda DAR. Habari ambazo bado kuthibitishwa zinasema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na kondakta kwa mwendo wa kasi sana. Hayati Kabuye alikuwa njiani kuhudhuria mkutano mkuu wa TLP.
baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo
mmoja ya waliopoteza maisha
wasamaria wema wakisaidia majeruhi

Globu ya Inawezekana inatoa rambirambi kwa wafiwa katika ajali hii na pole kwa majeruhi. Wakati huo huo inaweka alama ya kujiuliza kwa nini hizi ajali hazikomi. Tatizo ni nini hadi ndugu zetu wanateketa namna hii kila kukicha? Kifanyike nini ili balaa hili lituame?

No comments: