Monday, July 27, 2009

ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni
Babu wa Miaka 77 Ajibadilisha Jinsia kuwa Mwanamke




Babu Richard Ramsey mkazi wa Philadelphia nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 77 amekuwa mtu wa kwanza duniani kubadilisha jinsia yake akiwa na umri mkubwa kama huo.

Ramsey wakati wa ujana wake aliwahi kuwa miongoni mwa wanajeshi wa Marekani waliopigana vita vya Vietnam na kufanikiwa kurudi Marekani salama.

Ramsey alifanya kazi jeshini kwa miaka 20 na alioa na kuacha mara mbili.

Ramsey amedai kuwa tangia alipokuwa na umri wa miaka 13 alianza kujihisi kama mwanamke lakini kutokana mazingira aliyokuwa akiishi chini ya wazazi wake ambao walikuwa ni watu wenye msimamo wa maadili aliendelea kuzificha hisia zake kama siri yake.

Ramsey hivi sasa akiwa na umri wa miaka 77 ameamua kuzifata hisia zake na kufanya operesheni ya kujibadilisha jinsia kuwa mwanamke kwa kuondoa nyeti za kiume na kupandikizwa nyeti za kike.

Operesheni hiyo ya kubadilisha jinsia ilimgharimu Ramsey dola 20,000 za Marekani.

Madaktari walisema kwamba Rene alikubali kufanya upasuaji wa kubadilisha jinsia yake pamoja na kuambiwa kuwa operesheni hiyo ingeweza kumsababishia madhara kwenye mwili wake kutokana na umri wake mkubwa.

Richard Ramsey amejibadilisha jina lake baada ya operesheni hiyo na kujiita Renee Ramsay.

"Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu najihisi kama hisia zangu zilivyokuwa zikinituma" alisema Rene na kuongeza "Kubadilisha jinsia lilikuwa ni jambo nililolidhamiria kulifanya siku nyingi kabla sijafariki".


No comments: