Wednesday, July 15, 2009

kipaji kingine cha soka ughaibuni chavumbuliwa
Juu na chini ni mchezaji wa kibongo Denis Geoffrey (jezi nyeupe) mwenye mpira katika majaribio nchini Puerto Rico na timu ya Carolina Cigantes

Mchezaji Denis Geoffrey ni miongoni mwa wachezaji wenye ndoto ya kucheza mpira wa kulipwa nje ya Tanzania,Denis alizaliwa Tanzania,mkoa wa Arusha miaka 24 iliyopita.sasa hizi anaishi nchini Marekani,Durham,North Carolina na anachezea timu ya Cary Clareps inayoshiriki ligi inayoitwa USL.

hii timu ipo chini ya ajenti anayeitwa Howid Goldberg anayeandaa vijana wenye vipaji kama Denis na hatimae kuwatafutia timu ya kulipwa hapa marekani na hata ulaya.

Howid Goldberg pia ni ajenti wa mchezaji Nino Gomez anayechezea Fc Porto ya Ureno.Denis anasema kutokana na yeye kua na kipande cha kijani ndio maana kwake ni vigumu kwa ajenti kumpa majaribio ulaya.

Denis alikuja huku Marekani akiwa na miaka 14 kwa kumfuata Baba yake Lepana Geoffrey na amesoma na kucheza mpira college ya Columbia,St.Louis 2005-08,mwenyewe pia anapendelea kufanya majaribio na timu ya Taifa kama atahitajika au kupata nafasi kufanya hivyo.

kwa habari zaidi za Denis unaweza kuzipata kwa kubofya www.caryclareps.com

No comments: