Wednesday, July 29, 2009

DAWASCO MAMBO MSWANO
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom Ephraim Mafuru akizungumzia huduma ya kulipia maji kwa kutumia huduma ya simu ya mkononi M-Pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ofisi za Dawasco jana.waliokaa katika ni Mkurugenzi wa biashara wa Dawasco Raymond Mndolwa na Meneja habari wa DAWASCO Shabani Salum.

WATEJA WA DAWASCO SASA KUWEZA
KULIPA BILI ZAO KUPITIA VODAFONE M-PESA

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa mara nyingine imewawezesha wateja wake kulipa bili za maji kupitia Vodafone M-Pesa.Kwa sasa wateja wa vodacom wamewezakulipa bili zao za maji kwa kila mwezi kupitia Vodafone M-Pesa.Ni siku chache tu tangu kutangazwa kwa malipo ya LUKU kupitia Vodafone M-Pesa.

Mkurugenzi Masoko wa vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema katika makao makuu ya DAWASCO, kuwa kwa niaba ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Tungependa kuwakaribisha DAWASCO katika ulimwengu wa Vodafone M-Pesa. Vodafone M-Pesa ilianzishwa mapema mwaka jana(2008) kama huduma ya kusafirishia pesa kutoka kwa mtu mmoja kuelekea kwa mwingine.Huduma hii imeendelea kukua na kupanuka hadi kuwawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili,ada za shule na ulipaji wa mikopo.

Vodafone M-Pesa ni njia rahisi ya kutuma hela kwa kutumia simu za mkononi.Mtandao huu wa Vodacom M-Pesa uliyowawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili zao za maji DAWASCO.

Mafanikio ya huduma hii yamefanikiwa kwa ushirikiano baina ya Vodacom Tanzania na DAWASCO.Kwa Kampuni hii ya simu za mikononi ya Vodacom tunajua huu ni mwanzo tu, Bado tutaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika mengine katika kukuza na kutoa huduma hii kwa ubora zaidi kwa wateja wetu.alisema Mafuru

Akiongelea huduma hiyo Afisa biashara wa DAWASCO Raymond Mndolwa amesema, Sisi kama DAWASCO tutaendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu kupitia mitandao tofauti ya mawasiliano.

Tunatumai wateja wetu watafurahia kutumia huduma hii ya kulipa bili ambayo itarahisisha maisha Yao.

DAWASCO imeahidi uboreshaji
zaidi katika huduma zao

No comments: