Saturday, July 25, 2009

libeneke la NMB mobile
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ben Christiaanse akizindua NMB Mobile
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Imani Kajula akiwa na maafisa wengine wa NMB. Mkuu wa wateja binafsi Abdulmajid Nsekela, Mkuu wa Idara ya Uhusiano Shyrose Bhanji na Mkuu wa Fedha Waziri Barnabas.


NMB YAZINDUA HUDUMA ZA KIBENKI KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI-NMB mobile.

Banki ya NMB imeweka historia nchini Tanzania kwa kuzindua huduma ya NMB mobile inayomuwezesha mteja kupata huduma za kuangalia salio, kutuma fedha, kuangalia statimenti fupi, kununua luku, na muda wa maongezi wa Vodacom au Zain.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa NMB mobile, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ben Christiaanse alisema ‘’ Hii ni hatua kubwa kwa NMB na wateja wake kwani sasa wateja wana wigo mpana wa kupata huduma na pia kuokoa muda, fedha na adha ya foleni’’. Mwaka 2006, NMB iliandaa mkakati wa miaka mitano wa kuboresha huduma. Hadi sasa NMB ina matawi zaidi ya 130, ATM zaidi ya 210 Nchi nzima. NMB inatazamia kuwa na ATM zaidi ya 270 ifikapo mwisho wa mwaka 2009.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula akielezea faida za NMB mobile alisema ‘’ NMB mobile inawezesha wateja wa NMB Personal Account, NMB Student Account na NMB Wisdom Account kupata huduma za NMB popote walipo wakati wowote na kwa gharama nafuu. ‘’
Kujiunga na huduma ya NMB mobile ni rahisi na haihitaji mteja kwenda kwenye tawi la NMB, unachotakiwa kufanya ni kupiga namba *155*66*123# kisha fuata maelekezo”.
Huduma ya NMB mobile inapatikana kwa wateja wa NMB wenye mitandao ya ZAIN na Vodacom. NMB inategemea kuwezesha huduma hii kupatikana kwa kutumia mitandao mingine pia.

No comments: