Wednesday, July 22, 2009

Ras Makunja na Ngoma Africa aka FFU katika makamuzi ya hasira!ndani ya Fest-Africa,Finland.



Mwanamziki Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu na mzimu wake FFU ,juzi jumamosi walifungua ukurasa mpya katika jukwaa la Fest-Africa,kwani waliweza kuwapa burudani ya aina washabiki wa ufini,
wanamziki washambuliaji (FFU) wa safu ya mbele waliweza kuwamdudu washabiki vizuri,Ras Makunja kiwaongoza jukwaani washambuliaji wake wa safu ya mbele mpiga solo Chris-B,ambaye pia anaimba na Bi.Severne aka Sevasha au afande wa kike,huku mdundo mkali wa The Ngoma Africa Band ukiwasindikiza na kuweza kufanikiwa kuwayumbisha washabiki katika onyesho hilo!
Kitu cha kufurahisha mziki huo wa Ngoma Africa uliweza kuwazoa washabiki na kupanda jukwaani kusakata ngoma za moto! na mziki huo kuonekana kuwa una nguvu zaidi ya kuwanasa na kuwatia kiwewe
washabiki katika maonyesho mengi barani ulaya.
Mafanikio haya ya Ras Makunja na bendi yake "The Ngoma Africa "yanaonyesha wazi kuwa Tanzania ina utajiri wa wanamziki wanye uwezo na vipaji vya kuitangaza tannzania nje ya nchi,hila wanakosa msukomo fulani kutoka kwa tahasisi na pengine sisi watanzanian wenyewe.
Ras Makunja na mzimu wake au bendi yake The Ngoma Africa,bendi ambayo pia inajulikana kama "The Golden Voice Of East Africa" au kama wengi walivyoipachika jina FFU fanya fujo uone,ni bendi hiliyojijengea jina na kujizolea umaarufu barani ulaya na katika kona zingine duniani kutokana na ukali wa mdundo wake wa dansi,mdundo ambao mara nyingi una nguvu ya kasi ya kuweza kuwazoa na kuwatia kiwewe washabiki! Pia wanamziki wa bendi hiyo wawapo jukwaani inaonyesha wazi kuwa mziki wao ni mkubwa na pia wapo imara katika kulimudu jukwaa na washabiki.
labda tujaribu kuwasikiliza hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica ukiwahitaji wanapatikana hapa ngoma4u@googlemail.com

No comments: