Friday, January 1, 2010

SALAAM TOKA KWA CHEF ISSA

KARIBUNI SANA KATIKA
LIBENEKE LA MAPISHI NA CHAKULA

Ndugu zangu namshuku sana mwenyezi mungu kwakuniwezesha kumaliza masomo yangu salama Pia natoa shukurani zangu za dhati kwa mke wangu kipenzi na mwanagu, wazazi na ndugu zangu kwa sapoti yenu kubwa.

Mimi chef Issa nimeamua kuanzisha libeneke la fani ya chakula ambapo wale wote wenye taaluma hii na wapenda chakula cha aina yeyote watapata fursa ya kujifunza kutoa maoni na kufundisha pia mapishi ya aina mbali mbali

Tutakaribisha pia recipe mbalimbali toka kwa yeyote atakaye penda kuchangia mawazo lengo ikiwa ni kubadilishana ujuzi ili kila mmoja wetu afaidike na utaalamu husika. Mapishi ya ladha zote mchango wowote ule utaheshimiwa sana.

Tutakua na historia ya vyakula toka mataifa ya ulaya magharibi ambayo ni maarufu kwa vyakula vyao toka enzi hizo vikipikwa kwa mtindo wa zamani tuliouzoea na pia vikibadilishwa kwa mtindo mpya wa kisasa vikibaki na majina yaleyale hubadilika kwa kunakishiwa kwa mitindo mbalimbali.

Pia tutapata wasaa wa kujua historia ya vyakula na utambulisho kinatoka nchi gani na hasa tutagusa mataifa mama kwa nchi za magharibi katika sanaa hii ya chakula ikiwa ni Spain, England, France, German, Austria, Switzerland na Italy.

Tutaangalia pia utaalamu, sifa na aina za cheese, utundu wa kutengeneza na kunakshi chocolate na historia yote kwa ujumla. Pia tutapata nasaha ya kuona vifaa mbalimbali na kujifunza kuchonga matunda na mboga ktk maumbile tofauti mfano tunda kama apple unatengeneza bata mzinga inapendeza sana hakika ushirikiano wenu ndugu zangu utaifanya blog hii iwe chuo bora cha kubadilishana utaalamu wa fani hii ya chakula.

Kwa sasa nakaribisha maoni yenu na tuanze na nini baada ya maelezo yote hapo juu ili blog hii iboreshwe zaidi na kila mmoja wetu afaidi?

Pia nashughulikia uwezekano wa kufundisha kwa njia ya video hapa hapa katika blog yetu. wadu wote na ma chef wenzangu wazalendo karibuni sana sana sana katika Libeneke hili la chakula.

Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2010 cheers!! http://www.activechef.blogspot.com/
CHEF ISSA

No comments: