Saturday, January 2, 2010

Jinsi alivyokuwa mwaka 2003
Ndege iliyonusulika kulipuliwa
Babake mzazi, Alhaji Umaru Mutallab
Farouk na mama yake mzazi inavyosemekana
Nyumba ya kifahali aliyokuwa anaishi London
Uwanja alioanzia safari yake Nigeria
Baba wa kijana ambaye alitaka kulipua ndege iliyokuwa imewabeba abiria karibu 300, alionya Marekani kuhusu vitendo vya mwanawe na hasa msimamo wake mkali wa kisiasa.

Babake mzazi, Alhaji Umaru Mutallab, ambaye ni mfanyibiashara maarufu nchini Nigeria alikuwa ametoa ripoti kwa ubalonzi wa Marekani jijini Abuja.

Mnamo michache iliyopita alielezea wasiwasi wake kuhusu msimamo mkali wa kisiasa wa mtoto wake ambaye anasomea uhandisi kwenye chuo kikuu kimoja mjini London, University College London.

Kutokana na jaribio hilo mnamo siku ya Krismasi, usalama umeimarishwa katika viwanja mbalimbali duniani kote.

Kijana huyo amefunguliwa mashtaka akiwa hospitalini Michigan ambako amelazwa na majeraha ya mguu aliyopata alipojaribu kuwasha mabomu ambayo alikuwa amejifunga mwilini na kwenye suruali yake ya ndani.

Wakati akijaribu kujilipua, abiria wenzake na wahudumu wa ndege walimwandama kwa nguvu huku ndege hiyo iliyokuwa imesafiri kutoka Uholanzi ikijiandaa kutua mjini Detroit, Marekani.

Familia ya kijana huyo pia iliilezea Idhaa ya Hausa ya BBC kwamba hawakuwa tena na mawasiliano na mtoto wao tangu mwezi Oktoba alipokuwa akiishi Yemen.

Inaripotiwa kwamba aliondoka Yemen akaelekea Ethiopia, halafu Ghana na kisha Nigeria.

Bado kuna maswali mazito kuhusu jinsi Mutallab ambaye ana Visa halisi ya kusafiri hadi Marekani, alivyopanda ndege kutoka Lagos hadi Amsterdam licha ya kuwepo na taarifa kuhusu vitendo na mienendo yake.

No comments: