Thursday, January 28, 2010

BREKING NYUUUUZZZZ: WANAJESHI WANAOTUHUMIWA KUMUUA SWETU WATINGA MAHAKAMANI KISUTU JANA

Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya marehemu Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakisindikizwa kuelekea chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar mchana jana.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira, marehemu, Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakiwa katika chumba cha Mahakama jana.
Ndugu wa marehemu, Swetu Fundikira wakiwa nje ya mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi ya mauaji ya ndugu yao ikiwa inaendeklea.

Kushoto ni Nzwala Fundikira na kulia ni Ismail Fundikira.



Washtakiwa wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala

Mh. Dudu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba kwa mujibu wa kosa linalowakabili hawatakiwi kujibu chochote na kwamba kosa hilo halina dhamana kwa sababu hiyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kuairisha kesi hiyo Februali 10 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa. Akaamuru washitakiwa wote wapelekwe rumande.


Ndugu wa marehemu Swetu walikuwepo mahakamani na kusikiliza kesi kwa utulivu, huku wakisema wana imani kwamba haki itatendeka.


Swetu Fundikira alifariki dunia Jumapili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa toja Ijumaa usiku baada ya kupigwa sana na wanajeshi watatu, wawili wakituhumiwa kuwa ni hao pichani na mwingine wa tatu haijulikani alipo na msako unaendelea.


Marehemu Swetu alizikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar. Kifo chake kimezua zogo kubwa miongoni mwa wananchi ambao wanadai uongozi wa majeshi yote ya ulinzi na usalama uwe wakali kuhakikisha askari wachache wenye mtindo wa kutokuwa na nidhamu hawapewi nafasi ya kuchafua majina mazuri waliyo nayo pamoja na ushirikiano mwema kati yao na jamii.




No comments: