Friday, January 1, 2010

msiba wa simba wa vita, ratiba ya mazishi
Mkuu Mkoa wa Dar es salaam, William Lukuvi akimfariji mke wa Marehemu Rashidi Mfaume Kawawa, Asina Kawawa, wakati alipoitembelea familia ya marehemu nyumbani kwa marehemu Madale jana jioni
Katibu Mkuu wa CCM, Yusu Makamba (kushoto) akimlilia Mzee Rashid Kawawa wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Madale jijini Dar jana jioni.

katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba akimfariji Zainabu Kawawa mtoto wa Simba wa Vita marehemu, Rashidi kawawa, Madale jana jioni.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, William Lukuvi akimpa pole Mh. Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo, Songea) ambaye mtoto wa Marehemu Rashid Kawawa nyumbani kwa marehemu Madale, jijini Dar jana jioni.

RATIBA YA MAZISHI YA SIMBA WA VITA

Mazishi ya Simba wa Vita Mzee Rashid Mfaume Kawawa yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi nyumbani kwa marehemu Madale jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba fupi iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa dar es salaam, Mh. William Lukuvi amesema jioni jana kuwa siku ya ijumaa mwili wa marehemu utapelekwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya wananchi kutoa heshima za mwisho.
Mh Lukuvi amewataka wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuanzia majira ya saa saba mchana kumuaga Simba wa Vita.


No comments: