Friday, October 16, 2009

wasanii wamuenzi mwalimu kwa kufanya usafi nyumbani kwake msasani
wasani wa tasnia ya filamu na muziki walikusanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Msasani, Dar, na kufanya usafi kuadhimisha miaka 10 ya kifo chake. Shughuli hii iliratibiwa na African Stars Entertainment, wamiliki wa bendi ya Twanga Pepeta, chini ya Mkurugenzi wake Da'Asha Baraka akisaidiana na Mamaa Dotnata, pamoja na kikosi kizima cha twanga pepeta na mastaa kibao wa filamu. Shughuli ilifana sana Mjukuu wa Mwalimu, Fortunata Nyerere, aliwashukuru wasanii hao kwa niaba ya familia
aisha madinda alikuwa mmoja wa wasanii waliofaidika na matunda ya Baba wa Taifa kwa kujipatia mzigo wa nazi kwenye bustani ya nyumbani kwa Mwalimu
Mamaa Dotnata akiwa kazini
Dk. Cheni alishughulikia taa za bustanini
JB naye alikuwa bize kutwa nzima kubeba taka

anko alikuwepo. hapa anakula konozzz na lillian internet, Lwiza Mbutu, Janet Isinike na paparazzi Muhidin Sufiani
wanenguaji wa twanga wakipepeta takataka zote
Mjukuu wa Mwalimu, Fortunata Nyerere, akiwashukuru wasanii hao kwa niaba ya familia
baadhi ya wasanii hao wakipozi baada ya kazi


Ujumbe: Mtandao wa
http://www.dailynews-tsn.com/
umetoa toleo maalumu la kukumbuka siku hii adhimu

No comments: