Friday, October 16, 2009

JK akiwa Musoma
Juu na chini kijana Mlemavu, Eliabu Buliro Kamoga akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya sanamu yake, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati kijana huyo alipokuja kumuona Rais Kikwete ikulu ndogo iliyopo mjini Musoma,Mkoani mara.Kijana huyo ambaye alisema yeye ni yatima alimwomba Rais Kikwete ampatie msaada wa usafiri kutokana na hali yake ya ulemavu na msaada wa kulipiwa karo ya masomo ambapo sasa hivi anasoma katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru,Mkoani Arusha kwa kulipiwa ma wafadhili mbalimbali na kutokana na kazi zake za sanaa.Pembeni anayeangalia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Mara Enos Mfuru.

JK akipandisha bendera ya CCM muda mfupi baada ya kufungua Tawi la Wanachama CCM wa Maisha Plus, Kitaji,katika Manispaa ya mji wa Musoma.

No comments: