Tuesday, October 6, 2009

siku music mayday walipopeleka fiesta la dezo uswazi
Siku ya tarehe 25 mwezi wa 9 mwaka 2009, itabaki kuwa ya kihistoria kwa wadau lukuki waishio maeneo maarufu ya Barcelona yaliyopo mitaa ya Mabibo jijini Dar, kufuatia bonge la shoo baabu kubwa iliyofanywa na wasanii kibao underground wa fani mbalimbali kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na shughuli za maendeleo ya wasanii chipukizi hapa nchini la Music Mayday Tanzania.
Unaweza kufeli kabisa kuelewa jinsi mashabiki walivyomiminika kushuhudia laiv mashairi,vina na umahiri wa kuigiza toka kwa wasanii kibao wakiongozwa na The motherland laivu bendi inayoundwa na damu chipukizi za akina Rogers Lukas, Malfred, Kala Jeremiah na wenzao. ‘Kwa watoto ilibidi kuweka ulinzi maalum’.
Shoo hiyo iliyoandaliwa na Music mayday Tanzania chini ya wawezeshaji MASHUJAA GROUP, ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuendesha tamasha la kupiga vita matumizi na ubwiaji wa madawa ya kulevya hasa kwa vijana ambao kwa hakika ndilo taifa la leo. Hapa ni katika vikao vya vijana kujadili athari za madawa ya kulevya


Kusema kweli motherland ni noma. Watu walitamani kukwaa jukwaani kuwadedesha akina kala, hawa jamaa ni mfuniko ile mbaya. Hiki ndo kichwa cha Music Mayday ambacho ni Afisa wa miradi ya huduma kwa jamii, ambacho pia kilicheza big role katika kufanikisha tamasha hilo, anti Prisca. Anawashukuru wanajamii wote wa Barcelona kwa muitikio mkubwa walioonesha. Chini Kwa heshima na taadhima ilibidi watoto waachiwe jukwaa ili kuwapa shavu wasanii baada ya watoto hao kutaka kolabo na wasanii hao. Palikuwa hapatoshi.
Huku ndiko kuigiza, maana hawa jamaa wa Elizabeth theatre group waliact mpaka watu wakataka kutoa machozi. Usijaribu hawa wanaigiza tu, na kumbuka; ‘kuwa teja siyo Dili’.
Malfred ‘HUYU’ Kashikilia zawadi ya CD yenye albam yake kwa mtu ambaye angeweza kuimba nyimbo zake bila kuchapia.









No comments: