Thursday, October 8, 2009

Thabeet aanza ngwe ya awali NBA League

ANGALIZO. Hiyo si "tatoo", ni maandishi juu ya picha. Picha kwa hisani ya

www.memphisbluebears.com

Hasheem Thabeet, usiku wa kuamkia leo alifungua pazia la kushiriki mechi ya kwanza ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA pale alipoichezea timu yake ya Memphis Grizzlies dhidi ya Washington Wizards katika mechi ya kwanza kati ya mapambano ya kujipima nguvu kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa 64 wa ligi ya NBA utakaoanza rasmi Oktoba 27 2009 na kumalizika Aprili 14 2010.

Katika mechi hiyo ambayo Wizards walishinda 101-92, Hasheem alionekana kufanya vema kwa kuweza kufunga pointi 6 na kuzuia mitupo 4 ndani ya dakika 15. Huu si mwanzo m'baya kwa Hasheem ambaye alikuwa chaguo la pili kwa thamani katika draft ya NBA na sasa ameanza ngwe nyingine ya UCHEZAJI WA KULIPWA katika mpira wa kikapu.

Kila la kheri Hasheem
"
www.changamotoyetu.blogspot.com"

No comments: