Tuesday, December 23, 2008

KP NA BUSARA ZAKE !!!


zain yaja na internet ya megabit 7 ya 3.5G
mkurugenzi mkuu wa zain tanzania khaled muhtadi na bosi mwenzie wakionesha modem na simu zinazoweza kutumika kwa huduma mpya ya 3.5G iliyozinduliwa leo na kampuni hiyo
paparazi wakimpiga mande mkurugenzi mkuu wa zain tanzania khaled muhtadi alipokuwa akizindua huduma ya intanet ya kasi ya teknolojia ya 3.5G yenye spidi ya mebiti 7 katika hoteli ya kempinski, dar. tanzania na ghana pekee ndizo nchi zenye huduma ya 3.5G katika nchi 16 ambazo zain imesambaa
Matokeo ya darasa la saba 2008: Kiingereza, hisabati bado not richebo shule za msingi
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe akitangaza matokeo hayo

Asilimia 80.73 ya wanafunzi 433,260 waliofaulu darasa la saba wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za serikali ambapo wasichana ni 188,460 sawa na asilimia 82.13 na wavulana 244,800 sawa na asilimia 79.69 .

Akitangaza matokeo hayo jana mchana kwa waandishi wa habari, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe (pichani) alisema kuwa kati ya wanafunzi wote 1,017,967 sawa na asilimia 97.51 ya walioandikishwa walifanya mtihani huo mwaka huu na wanafunzi 536,672 sawa na asilimia 52.73 wamefaulu.

Katika matokeo hayo ambayo yataanza kutangazwa na kila mkoa kesho, wavulana walifanya vizuri zaidi ambapo walikuwa 307,196 sawa na asilimia 59.75 huku wasichana waliofaulu ni 229,476 sawa na asilimia 45.55.

Aliitaja mikoa iliyofanya vibaya na kiwango cha ufaulu kwa asilimia kwenye mabano ni Shinyanga(34), Lindi(40.7), Mara(42.6) na Tabora asilimia 43.2.Kwa Mikoa iliyofanya vizuri ni Dar es Salaam(73.9), Arusha(69.2), Iringa(64.1) na Kagera 63.5.

Kwa upande wa wanafunzi waliobainika kufanya udanganyifu alisema “watahiniwa 102 wamefutiwa mitihani wakiwemo wasichana 41 na wavulana 61”.

Akifafanua juu ya ufaulu wa masomo ya Hisabati na Kiingereza ambayo kwa miaka miwili mfululizo umekuwa wa chini, Profesa Maghembe alisema kuwa Hisabati ni asilimia 18.07 huku Kiingereza ni asilimia 31.5

Ameongeza: “matokeo ya Kiingereza ni sawa na mwaka jana na Hisabati mwaka jana ni asilimia 18.72, tumeweka mikakati ya kuboresha masomo hayo ikiwemo vyuo vyote vya ualimu kutoa nyenzo kwa wanafunzi wa ualimu kuweza kufundisha masomo hayo, kuwapa mafunzo walimu waliopo na tunatoa wito kwa wanafunzi wasiyaogope masomo haya”.

Ufaulu wa masomo mengine na kiwango katika asilimia ni Kiswahili(73.4), Sayansi(68.24) na Maarifa(61.03).
Waziri Maghembe alisema kati ya wanafunzi 346 wenye ulemavu waliofanya mtihani huo, wanafunzi 221 sawa na asilimia 64 ya watahiniwa wamefaulu na wote wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza.
THE ORIGINAL COMEDY WATUA KWA MAMA
PICHANI KUTOKA SHOTO: MUJUNI SYLIVESTER(MPOKI), EMMANUEL MGAYA(MASANJA MKANDAMIZAJI), JOSEPH SHAMBA(VENGU), MHESHIMIWA BALOZI MAMA MWANAIDI. S. MAAJAR, LUCAS MHUVILLE(JOTI), ALEX CHALAMILA(MAC-REGAN), NA ISSAYA MWAKILASA( WAKUVANGA)
THE ORIGINAL COMEDY WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BALOZI NA MAOFISA WENGINE WA UBALOZINI HAPO.

HABARI ZILIZOINGIA SASA HIVI NI KWAMBA WASANII WA KUNDI LA VUNJA MBAVU LA THE ORIGINAL COMEDY WAMETUA JIJINI LONDON KWA ZIARA YA SIKU KADHAA NA LEO MCHANA WAMETEMBELEA OFISI ZA UBALOZI .
WAKIWA UBALOZINI HAPO WALIPATA NAFASI YA KUONANA NA KUONGEA NA MHESHIMIWA BALOZI, MAMA MWANAIDI SINARE MAAJAR PAMOJA NA MAOFISA WENGINE WA UBALOZINI HAPO KUHUSU UTENDAJI WAO WA KAZI NA MASUALA MENGINE MUHIMU KWA JAMII.
HABARI ZAIDI ZA ZIARA HIYO ZITAFUATA BAADAYE.

hotuba ya mwalimu nyerere huko chimwaga, dodoma, mwaka 1995
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Video ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipozungumza na WanaCCM mwaka 1995 katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi huko Chimwaga, Dodoma, kwenye mchakato wa kumtafuta mgombea wa kiti cha uraisi awamu ya tatu kwa tiketi ya CCM. Wagombea watatu, Benjamin Mkapa, Cleopa Msuya na Jakaya Kikwete walipitishwa na hatimaye Mh. Mkapa akashinda kugombea urais.


Msikilize Mwalimu kwa kubofya link hii

Saturday, December 20, 2008

EBU ONA MAAJABU YA DUNIA!!


MTU HUYU ALIAMUA AZIKWE NA VITU VYAKE,:
PLASMA TV YAKE, KABATI LAKE, DRESSING TABLE YAKE, KITANDA CHAKE, WHISKY ZAKE, DVD PLAYER YAKE…NAKADHLIKA, HEBU JIONEE MWENYEWE HILO KABURI
.
Mrocky Mrocky atunukiwa
Nishani...


Mpiga picha wa Daily News,Bw Mroki Mroki(Kushoto) ametunukiwa nishani ya Anjouan, kutokana a mchango wake katika kuhabarisha jamii wakati wa mapambano ya kumng'oa kiongozi wa waasi nchini Comoro na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Nchini Mheshimiwa Bernard Membe.

Ndani ya nchi yetu ya Tanzania,Bw Mroki amekuwa ni mmoja wa wapiga picha walio mstari wa mbele katika kutuhabarisha kuhusu matukio mbali mbali yanayohusu maisha ya kila siku ya Mtanzania.Kutafuta kwake habari kumemfanya mara nyingine apate misukosuko katika kazi hii.Nakumbuka mara ya mwisho ni ile tafrani iliyotokea katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria.
kwa niaba wa wadau wote wa blog hii tunapenda kumpongeza Mdau Mrocky Mrocky
Mheshimiwa Temba Afanya
Kweli...
Mheshimiwa Temba kutoka kundi la muziki wa kizazi kipya wa TMK Wanaume Family,Jumamosi iliyopita aliamua kuachana na ukapera baada ya kufunga pingu za Maisha katika kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.Picha Zote kwa Msaada wa Mdau Abdallah Mrisho Salawi
kp na Bush !!!!!!!!!
Blogu Ya Nyimbo Za Dini
Baada ya kuchoka kukimbia huku na huko mtandaoni kusaka nyimbo za dini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya (2009), nimeamua kuanza kuzikusanya na kuziweka nyimbo mbalimbali za dini katika blogu hii: nyimbozadini.blogspot.com Nachukua nafasi hii basi kuwakaribisha wadau wote wanaopenda kusikiliza nyimbo za dini kuitembelea blogu hiyo. Ni lazima niseme pia kwamba ndiyo tu nimeianzisha blogu hii na kutokana na pilipilika kuwa nyingi sijapata muda hasa wa kuishughulikia ipasavyo na kwa hivyo uchanga wake unaonekana wazi. Maoni ya jinsi ya kuiendeleza zaidi yanakaribishwa. Blogu yangu ya kiuchambuzi wa kiundani kabisa wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yetu inakuja hivi karibuni.

Natanguliza shukrani zangu

Mwalimu Masangu Matondo Nzuzullima