Wednesday, July 30, 2008

Sumaye Atoa Siri....
Sumaye Atoa Siri....

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametoboa siri nzito ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa,jinsi alivyomteua mara mbili kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa waziri mkuu pekee aliyelitumikia taifa kwa mihula miwili mfululizo.

Sambamba na hilo,Sumaye alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini, anamshukuru Mungu kwamba alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.
Sumaye alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na kipindi cha ‘Jicho Letu’ wiki hii, kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM.Mahojiano hayo ya Sumaye, yanatarajiwa kurushwa na kipindi hicho Jumamosi ijayo.

Bila kufafanua kwa undani,Sumaye alisisitiza kuwa kwa jinsi hali ya mambo inavyokwenda kiuchumi,kisiasa na kijamii,hajutii kabisa kuikosa nafasi hiyo iliyokutanisha wagombea wengine 11 kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM)na hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete,kuibuka mshindi.

Katika mahojiano hayo,Sumaye alitoboa siri ya mshituko alioupata siku alipoitwa na Rais mstaafu Mkapa,na kujulishwa nia ya kutaka kumteua ili awe waziri mkuu.‘‘Kusema ukweli, sikuwa na habari hadi saa 7:30 ya siku ya uteuzi,ndipo Rais Mkapa aliponidokeza nia yake ya kutaka niwe waziri mkuu.Sikutegemea wala sikuota kama naweza kuwa waziri mkuu na hakuna mtu yeyote aliyejua mpango huo,kwani hakuna habari zilizovuja kabla,” anasema.

Alisema siku hiyo,akiwa nyumbani kwake amejipumzisha,alipata taarifa za kuitwa Ikulu na Rais Mkapa.‘‘Wala sikutegemea habari ya kuwa waziri mkuu,maana hata Mkapa mwenyewe sikuwa nimezoeana naye,”alisema.
Bofya na endelea>>>>>
Vichwa Vya Magazeti Mbalimbali
Jana Bongo...

MWANAJESHI AMUUA MKEWE
KWA RISASI LUGALO..
---------
ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA -JWTZ KIKOSI CHA LUGALO ANADAIWA KUMUUA KWA RISASI MKEWE USIKU WA KUAMKIA LEO.HABARI TOKA NDANI YA KIKOSI HICHO ZINAMTAJA ASKARI HUYO KWA JILA LA ZUNGU AMBAYE ALIKUWA ANAFANYA KAZI KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA LUGALO.
IMEFAAHAMIKA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOVI WA KIMAPENZI ULIOTOKANA NA ASKARI HUYO KUFUMANIA SMS ZA MAPENZI KATIKA SIMU YA MKEWE SIKU KADHAA ZILIZOPITA NA ALIMFUKUZA MKEWE HUYO NA KWENDA NYUMBANI KWAO NDANI YA KIKOSI HICHO.
JUMATATU USIKU ALIMUITA AKIWA LINDONI KATIKA GETI DOGO LA KUINGILIA HOSPITALINI HAPO NA KUMSHAMBULIA KWA RISASI TANO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.ASKARI HUYO ANADAIWA BAADA YA KUMALIZA KAZI HIYO ALIAGIZA MAJI YA KUNYWA NA KUSHUSHIA KABLA YA KUSALIMISHA SILAHA KWA WENZAKE AMBAO WALITAKA KUTIMUA MBIO ALIPOKUWA AKIWAFUATA.HIVI SASA ZUNGU ANASHIKILIWA NA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAHOJIANO ZAIDI.HABARI NA MROCKY MROCKY.
Mzee Bhoke Munanka
Azikwa Jana..
Hayati Isaac Bhoke Munanka Enzi Za Uhai Wake.
Rais Mstaafu Mzee Benjamini Mkapa na aliyekuwa Waziri Mkuu,Mh Edward Lowassa wakiwa kwenye msiba nyumbani kwa marehemu Mzee Munaka Kimara Baruti jijini Dar es Salam jana
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mohammed Abood(Kushoto)akiwa na wambolezaji wengine jana nyumbani kwa Marehemu Mzee Munanka,Kimara Baruti jijini Dar es Salaam.
Ndugu na jamaa wa Marehemu Bhoke Munanka wakiomboleza kifo cha ndugu yao huyo kabla ya kuzikwa jana jioni jijini Dar es Salaam.
Wake wawili wa marehemu Munanka wakifarijiwa na ndugu na jamaa kabla ya kuuaga mwili wa Mzee Munanka ulizikwa jana jioni kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
----------
Waziri wa Nchi wa zamani katika baraza la kwanza la mawaziri wa Serikali ya awamu ya kwanza Mh. Isaac Bhoke Munanka aliyefariki dunia Jumamosi iliyopita akiwa na umri wa miaka 81 na kuzikwa jana katika makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es Salaam.Matanga yapo nyumbani kwa marehemu huko nyumbani kwake Kimara.Picha zote na Mdau Kassim Mbarouk
Tigo Wadhamini Nane Nane
Meneja wa Kampuni ya Tigo kanda ya kati na kusini,Willy Magehema (Kulia)akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,William Lukuvi simu ya mkononi baada ya mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma hivi karibuni juu ya udhamini wa kampuni hiyo katika maonyesho ya Nane Nane kitaifa yatakayofanyika mjini Dodoma kwa miaka mitatu mfululizo.

Tuesday, July 29, 2008

Kijana anayetuhumiwa kula watu acharuka mahakamani
Na Nora Damian

MTUHUMIWA Ramadhani Mussa (18), anayedaiwa kumuua mtoto Salome Yohana (3), jana aliuohoji upande wa mashitaka sababu za kuchelewesha upelelezi wa kesi yake.

Baada ya Ramadhani kupandishwa tena kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mwendesha Mashitaka Hudson Nduysepo alieleza kuwa upelelezi wa shitaka hilo bado haujakamilika.

Mara baada ya Mwendesha ashtaka huyo kutoa maelezo hayo na kabla hajaruhusiwa na hakimu Ramadhani alisimama na kuhoji sababu za upelelezi wa kesi inayomkabili yeye na mama yake Hadija Ally (38), kuchukua muda mrefu kukamilika. Pia alitaka alezwe ni lini upelelezi huo utakamilika.

''Kila siku tukija mahakamani tunaambiwa upelelezi bado, je utakamilika lini,'' alihoji Ramadhan.

Hakimu Euphamia Mingi anayesikiliza kesi hiyo alimtaka Ndusyepo kujibu hoja hiyo, naye akaeleza kwamba upelelezi unachukua muda mrefu kwa sababu kesi hiyo ni tofauti na kesi nyingine za kawaida ambazo upelelezi wake unatakiwa ukamilike ndani ya siku 60.

''Endelea kuwa mvumilivu kwa sababu kesi hii ni ya mauaji na lazima tufanye upelelezi kwa kina, ili kuhakikisha tunazitendea haki pande zote mbili,'' alisema Ndusyepo.

Wakati Ramadhani akihoji hayo, mama yake alikuwa amekaa kimya. Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alionyesha kutoridhika na maelezo hayo.

''Kwa hiyo inawezekana mkatumia hata miaka 60 mnafanya upelelezi. Kwanza mimi sijaua, lakini kila siku mnanileta mahakamani na kunirudisha, ni afadhali msinilete mpaka mkimaliza upelelezi wenu ndiyo mnilete hapa,'' alisema Ramadhan.

Hakimu Mingi baada ya kusikiliza hoja zote aliuagiza upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 11, mwaka huu itakapotajwa tena.

Ramadhan alikamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akidaiwa kwamba alikuwa amebeba kichwa cha marehemu Salome Yohana (3).

Awali ilidaiwa katika mahakama hiyo Aprili 24, mwaka huu kwamba majira ya usiku mtuhumiwa alimuua mtoto huyo katika eneo la Segerea kwa Bibi, jijini Dar es Salaam.
crdb yazawadia wanafunzi bora dodoma
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, William Lukuvi (kulia kwake) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei (watatu kulia) wakiwa na wanafunzi watatu wa darasa la saba waliofanya vizuri katika somo la Hisabati mkoani Dodoma katika sherehe za kuwazawadia 9533 wanafunzi waliofanya vizuri katika somo hilo zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wiki iliopita. Wanafunzi hao kutoka kushoto ni Sharifa Hamisi wa Shule ya Misngi Pandambili, Kongwa , Sharifa Hamisi wa Shule ya Msingi,Mtengete ya Mpwapwa na Said Suleiman wa Shule ya Misingi Karamba , Kondoa
matukio fainali za kombe la kagame cup 2008
balozi wa rwanda nchini akiwavisha medali washindi wa pili uganda revenue authority
wadau wa castle lager walikuwepo pia
trupu la tbc one likirusha mambo laivu. kipa wa kimataifa wa zamani wa pan african juma pondamali 'mensah' (shoto chini) akiwa na juma nkhamia na crifford ndimbo wakifanya mambo
wanaume tmk walikuwepo kurusha mapanga yao shwaa shwaaa...
washindi wa tatu wa kombe la kagame cup 2008, wekundu wa msimbazi simba sc
mwenyekiti wa simba hassan dalali (mwenye kibandiko) akiwa na vingunge wa friends of simba


balozi wa kenya nchini mh. mbaya (mwenye miwani) akifurahia kombe la kagame na vijana wake wa tusker
warembo wa miss tz 2008 nao walikuwepo kushuhudia fainali za kombe la kagame cup






kocha wa tusker jacob 'ghost' mulee akionesha dola 30,000 keshi alizopokea kwa kutwaa ubingwa wa kombe la kagame cup 2008. rais paul kagame anatoa dola 60,000 kila mwaka kwa ajili ya kombe hilo ambapo mshindi wa kwanza analamba hizo dola 30,000 wa pili anabeba 20,000 na wa tatu anatia kibindoni dola 10,000. tanzania breweries kupitia kilaji chake cha castle lager wametoa milioni 80 pamoja na jezi na vifaa kama wadhamini wakuu
nahodha wa simba akionesha dola 10,000 walizovuna kama washindi wa tatu wa chee baada ya yanga kuingia mitini

washindi wa pili uganda revenue authority kabla ya mchezo wao na tusker waliolala 2-1
waamuzi wa uliokuwa mpambano wa simba na yanga wakipiga jalamba kabla ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambao yanga hawakutokea uwanjani kwa sababu wanazozijua wenyewe


juu na chini ni mabingwa wapya wa kombe la kagame cup 2008 wakifurahia ushindi wao wa bao 2-1 dhidi ya uganda revenue authority



tusker fc kabla ya mchezo wao wa fainali


bosi wa biashara wa tanzania breweries limited david minda akiwavisha medali za ushindi wa tatu wachezaji wa simba sc
rais wa tff sir leodegar chilla tenga akiwavisha medali za ushindi wa pili uganda revenue authority

tunashukuru sana mzee wa fulanazzzzz kwa kazi yako nzuri yakutuhabarisha nakuona ulikuwepo kuleta vitu laivu toka neshno .
Adadi aagwa Rasmi Jeshi la
Polisi.
Pichani ni IGP Mstaafu Afande Omary Mahita(Kushoto)Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu na kulia Kabisa ni IGP/Mkuu wa jeshi la Polisi wa Sasa Afande Saidi Mwema.
Kutoka Habari Leo
--------------
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Adadi Rajabu, amemwomba Mkuu wa Polisi nchini (IGP),Saidi Mwema,kutoa kipaumbele katika Kitengo cha DCI kwa kuwa ndio uti wa mgongo na kitengo muhimu katika kazi za polisi.Akizungumza katika sherehe za kumuaga zilizoandaliwa na Polisi Kitengo cha DCI Dar es Salaam juzi.


Adadi ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe,alisema idara hiyo ndio inayobeba lawama zote za polisi pindi uhalifu unapotokea.“Idara hii pamoja na kazi ya ukachero ni ngumu na haiwezi kuendelea bila baraka za IGP,mimi nilikuwa namghasi sana bosi wangu Mahita(IGP mstaafu Omari Mahita),inafikia kipindi hadi tunanuniana kwa siku mbili,” alisema Adadi.
Makachero walaaniwa bungeni kwa uvamizi ofisi za Gazeti Mwanahalisi *Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu alipuliwa

*Ambiwa hana tija, upinzani wataka nafasi ifutwe

Na Ramadhan Semtawa, Dodoma

SAKATA la makachero wa Polisi kuvamia na kupekua ofisi za Kampuni ya Halihalisi Publishers, limeingia katika sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kulaani na kuitaka serikali itoe tamko kuhusu kitendo hicho.

Kauli za wabunge zitolewa wakati tayari wadau mbalimbali wamelaani kitendo hicho ambacho kinatishia uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Wabunge kwa nyakati tofauti, walitoa kauli hizo mjini hapa jana wakati wakichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni

na Michezo, kwa mwaka 2008/09.

Dk. Raphael Chegeni (Busega-CCM), alikuwa wa kwanza kulaani uvamizi katika ofisi hizo na kumpekua Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Saed Kubenea, akikiita kuwa ni chenye kutishia uhuru wa vyombo vya habari nchini. Kampuni hiyo mdiyo inachapisha magazeti la MwanaHalisi na Mseto.

Chegeni alifafanua kwamba vyombo vya habari katika siku za karibuni vimekuwa na mchango mkubwa katika kufichua uovu ikiwamo ufisadi uliofanyika katika mkataba wa Richmond na katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema ni lazima serikali ibadilishe mfumo wake wa utendajikazi na vyombo vya habari, ili kuweza kuondoa migongano isiyo na msingi.

''Nimesikitishwa na taarifa za kuvamiwa ofisi za gazeti la MwanaHalisi, vyombo vya habari vinafanyakazi nzuri, mambo ya EPA na Richmond yalianza kama rojorojo, na serikali iliwahi kukanusha ikisema ni uzushi tu, sasa haya mambo ya kupekuana ni kutisha waandishi,'' alisisitiza Dk Chegeni.

Hata hivyo, Dk Chegeni alionya na kukumbusha waandishi kufanyakazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao kwani kama watapotosha wataiweka jamii katika wakati mgumu na

kuivuruga nchi.

Alisema habari ni uchumi na kuhoji sababu za kupuuzwa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete,

ambalo liliweka utaratibu wa kutaka mawaziri kukunatana na waandishi kuzungumzia

mambo mbalimbali.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, aliunga mkono hoja hiyo huku akiitaka serikali kutoa tamko kuhusu makachero kuvamia na kupekua ofisi ya Halihalisi.

Zitto alisema ni vema Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, (George Mkuchuika), akatoa maelezo na kisha leo Waziri wa Mambo ya Ndani atoe kauli wakati akiwasilisha hotuba ya mapato na matumizi ya wizara hiyo.

Alisema kama uharaka uliofanywa na makachero kuvamia ofisi hiyo ungeelekezwa katika

vita dhidi ya ufisadi, basi kwa sasa ungekuwa unakaribiakwisha.

�Napenda nichukue fursa hii, kuungana na wenzangu wote kulaani nguvu za polisi kukamata na kupekua ofisi za Halihalisi na Mkurugenzi wake ndugu Kubenea, haraka na

nguvu hizi zingeelekezwa katika vita ya ufisadi, saa hizi ingekuwa

imemamalizika,� alisisitiza Zitto.

Zitto akichangia ukuaji wa uhuru wa vyombo vya habari, pia alitaka serikali ichague kufanya jambo moja kati ya mawili ambayo ni kutoa ruzuku ya asilimia 100 kwa Shirika la Utangazi nchini (TBC) au kulicha liwe huru kufanya biashara.

Mbunge wa Mchinga (CCM), Mudhihir Mudhihir, ambaye amekua kimya kwa muda mrefu katika mkutano wa 12 unaoendelea mjini hapa, aliibuka na kuchangia hoja huku akitumia misamiati na misemo mbalimbali ikiwemo ya Kiarabu.

Mudhihir alisema kilichopo sasa ni kwamba kuna vyombo vingi vinavyobika, ambavyo baadhi yao hutaka kupanda juu hata kuandika habari ambazo si sahihi.

Hata hivyo, alisema ni vema serikali ikawa na subira kwani chombo kimoja kikikosea si vyote na kuongeza: ''Padre mmoja akizini, si Ukristo wala Sheikh, Imam au Ustaadh, akizini si Uislam.''

Mudhihir aliendeleza hulka yake ya kutoa misemo kwa kusema, ''Kuna msemo kwamba, vijogoo vingihuharibu usiku, kuna vingine vitawika saa nne, lakini majogoo wa kweli watatulia, sasa hata magazeti yale ya kweli yatabaki tu.''

Awali katika hotuba mbadala ya kambi ya upinzani, iliyosomwa na Waziri Kivuli wa wizara hiyo Mwanawetu Said (Viti Maalumu �CUF), ililaani kitendo hicho na kuhoji vipi polisi ipoteze muda wa kukamata aliyetoa taarifa badala ya kufanya uchunguzi wa taarifa hizo.

Kambi hiyo pia ilimlaumu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, kwa kusema kazi ya kurugenzi yake hainonekani kutokana na tovuti ya Ikulu ambako ni ofisi ya Rais kutofanyakazi. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ni Salva Rweyemamu.

Msemaji huyo alisema tatizo hilo la tovuti ya Ikulu ni sawa na ile ya wananchi, ambayo huendeshwa na serikali kupitia Idara ya Habari (Maelezo), ambayo kwa muda wa mwaka mmoja sasa haifanyikazi na hata wananchi wakitaka kujibiwa maswali hayo hakuna

majibu wanayopata.

''Hatuoni umuhimu wa kuwepo Mkurugenzi wa Habari kama utendajikazi wake ndiyo huu,

tunashauri badala ya kuanzisha vyeo ambavyo havina ufanisi katika utendaji basi sasa

ni wakati wa kurudisha utamaduni wa kuwa na Mwandishi wa Habari wa Rais na majukumu

mengine chini ya wizara,'' alisema.