Saturday, October 9, 2010

service road barabara ya mandela road
Ankal pole kazi
Naomba kuuliza. Hivi hii sehemu ya barabara service road inamaanisha ku-service vimeo ama vipi. Mfano huyu jamaa ndo kageuza garage hapo. Naomba kugahamishwa
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

Monday, October 4, 2010

Ajali mbaya sana yatokea kinondoni jioni ya jumamosi.
Gari aina ya Subaru lenye namba za usajiri T 193 AZL ikiwa katika hali mbaya sana mara baada ya kupata ajali jioni ya jumamosi maeneo ya Kinondoni,Ubalozi wa Ufaransa.gari hii ambayo ilikuwa ikitokea maeneo ya Kinondoni Morocco kuelekea mjini,ilipoteza muelekeo mara baada ya gari moja kuingia ghafla katika barabara kubwa huku gari hii ikiwa katika mwendo wa kasi sana na kumfanya dereva wa gari hii kushindwa kuikontroo gari hii na kwenda kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani na kuifanya ikapinduka.ndani ya gari hii kulikuwemo na watu watatu ambao wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospital na mwingine kufanikiwa kutoka bila jeraha lolote.
Sehemu iliyokuwepo nguzo ya taa za barabarani iliyogongwa na gari hiyo na kuifanya ikang'oka kabisa katika sehemu yake.
Mmoja wa waliokuwemo ndani ya gari hiyo (anaetumia simu) ambaye hakutaka kutaja jina lake akijaribu kuwasiliana na ndugu na jamaa kuhusiana na ajali hiyo iliyowakuta.
Askari wa Usalama barabarani,akipata maenezo mafupi toka kwa mashuhuda wa ajali hiyo.

Sunday, September 26, 2010

Amazing Facts About Honey

Below are 10 amazing facts about honey that most people have no idea about. It is amazing what kind of health benefits can be found in foods given to us by mother nature herself. Simply adding natural foods like honey in place of more fattening options can make your body feel fresh and rejuvenated. Take a moment to read through all of these interesting facts about honey and see if you learn something interesting.
1. Honey is the only non man-made sweetener which also is considered to have healing effects.
2. Honey has a pH level around 3-4 and consists of roughly 18% water. Because of this honey is a very stable substance and can last hundreds of years if properly stored.
3. Honey can reduce fat deposits found in our cardiovascular system.
4. Honey will not ferment in your stomach like refined table sugar or sucrose does. Because of this it does not subject you to a risk of bacterial infection.
5. Honey is the simplest possible molecular form of sugar, which cannot be broken down any further. This allows it to travel directly from the small intestine to the blood stream while not causing any problems to the digestive system like sucrose.
6. Honey is a top choice as fuel for burning body fat during sleep since it has an equal ratio of fructose to glucose.
7. Honey is the best substance to use to treat burns. Honey can effectively subdue pain while quickly healing a wound without scarring.
8. Vitamins as well as antioxidants are found in honey. One special antioxidant known as ‘pinocembrin’ is found only in honey.
9. Honey is known to be a very effective and safe solution to children’s coughs, even more so than over-the-counter medicines.
10. Some recent studies have shown that athletes who consumed honey before and after physical activity have recovered faster than those athletes who did not consume any honey at all.
Given your new found knowledge of honey, now hopefully you can use it’s health benefits to your advantage. Keep in mind, the more natural the honey, the better. The honey found at your local fast-food chain is not going to give you the same health benefits as fresh natural honey straight from the bees nest. Start adding small amounts of natural honey to your meals to enjoy the health benefits it can offer you.

Wednesday, September 22, 2010

IBADA YA KUAGA MWILI WA ALIEKUWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. John Magufuli akitoa heshima za mwisho wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Dk. Ernest Mashimba aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza kwa Mazishi katika Kijiji cha Ngudu wilayani Kwimba.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Aisha Kigoda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba nyumbani kwake mtaa wa Ursino, Regent Estate, Dar es Salaam.
Mke wa aliekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali Marehemu Ernest Mashimba mama Rose Ernest akisaidiwa na ndugu wakati alipopita mbele ya jeneza la marehemu mume wake wakati wa kuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake jijini Dar es salaam, mwili wa Marehemu mashimba umesafirishwa Jana kwenda kijiji cha Ngudu Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi. Marehemu Ernest Mashimba alifariki wiki iliyopita Mkoani kwenye hoteli ya Executive Inn Lushoto mkoani Tanga alikokwenda kwenye mahafali ya mtoto wake Happy Ernest aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani humo.
Mtoto wa Marehemu aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani Tanga Happy Ernest Mashimba akiuaga mwili wa marehemu baba yake kwa majonzi makubwa.
UZINDUZI WA TAMKO LA WANAHARAKATI WASIO WA KISERIKALI 2010; “WAKATI UCHAGUZI NA BAADA YA UCHAGUZI 2010
Mgeni rasmi,Jaji Mstaafu Lameck Mfalila akionyesha kitabu cha tamko la Wanaharakati wasio wa Kiserikali 2010;“wakati na baada ya uchaguzi 2010:Tanzania ipi tunayoiitaka?”
Mgeni rasmi aliyezindua ni; Jaji Mstaafu Lameck Mfalila, Mwenyekiti wa Board, Agenda Participation 2000 pembeni akiangalia ni Resident Director-FES, Dr. Stefan Chrobot mwengine ni Balozi Mahmoud Jabir.

BOFYA HAPA
kwa habari kamili

Monday, September 20, 2010

dr slaa azidi kupasua na kampeni zake.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea ubunge katika jimbo la Hai kupitia chama hicho, Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa kampeni zilizofanyika Bomang'ombe mjini jana.
Waendesha pikipiki wakiwa katika maandamano ya msafara wa mghombea urais wa TanzaNia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kuelekea katika mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro jana. (Picha na Joseph Senga)
Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edwin Mtei, akiwahutubia wanachi wa Siha mkoani Kilimanjaro, wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (kulia) juzi. (Picha na Joseph Senga)

mgombea urais chama cha ccm mh jakaya kikwete alipounguruma manyara na babati

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete akiagana na wananchi kwa kuwapungua mkono, baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni , wilayani Babati.
Mgombea urais kwa chama cha CCM,Mh Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chipukizi wa Mkoa wa Manyara Hilda Prosper Hinghmaghway (7), anayesoma darasa la pili katika shule ya Rift Valley iliyoko Babati wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliohutubiwa na Mgombea urais kupitia chama hicho mjini Babati, (Picha na John Lukuwi).
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Jakaya Kikwete, akisalimiana na wananchi wa Haydom, mkoani Manyara, alipowasili katika mkutano wa kampeni, .(Picha na Freddy Maro.
eric shigongo aibuka na chuo kikuu cha mitaani

Mwalimu wa Kimataifa wa somo la Ujasiriamali, Eric James Shigongo amesogeza elimu nyumbani kwako na kukupa mafundisho yenye hadhi ya Chuo Kikuu cha Mtaani.

Shigongo atazindua CD inayoitwa Street University (Chuo Kikuu cha Mtaani) hivi karibuni, lengo likiwa kuwawezesha watu mbalimbali kujifunza somo la Ujasiriamali.Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Shigongo alisema kuwa ameamua kutoa CD hiyo ili kutoa fursa pana kwa wajasiriamali chipukizi kujifunza mbinu mbalimbali za kunufaika kibiashara.
“Ndani ya CD hiyo natoa elimu bora kabisa. Elimu ya kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa. Elimu ya kuwakomboa Watanzania katika mambo ya kiuchumi,” alisema Shigongo na kuongeza:“Nahitaji kuzalisha mabilionea wengi kadiri inavyowezekana, kwahiyo Watanzania wenye kiu ya kutaka kuwa mabilionea, wanaweza kunufaika kupitia CD yangu.”Shigongo aliendelea: “Watu wajiandae kuipata hivi karibuni. Itapatikana kwenye maduka ya Zizzou Fashions.”
JK ahudhuria mazishi ya julius msekwa jijini dar leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu JuliusMsekwa ambaye ni mtoto wa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwanyumbani kwao Bongoyo Oysterbay, jijini Dar asubuhi ya leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwamarehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCMBara Pius Msekwa wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwawazazi wa marehemu , Bongoyo Oysterbay jijini Dar es Salaam janajioni.Marehemu Julius Msekwa aliyefariki wiki iliyopita huko NicosiaCyprus ambapo alikuwa akifanya kazi ya mtaalamu Mshauri bingwa katikafani ya teknolojia ya Mawasiliano, alizikwa jana katika makaburi yaKinondoni jijini Dar jioni hii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,(wapili kushoto) Makamu Mwenyekitiwa CCM Bara Pius Msekwa(kushoto) na mkewe Mama Anna Abdallah(watatukushoto) pamoja na Rais mstaafu awamu ya tatu Mzee Ali HassanMwinyi(kulia) wakishiriki ibada ya mazishi ya kumuombea MarehemuJulius Msekwa aliyefariki huko Nicosia Cyprus wiki iliyopita nakuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar jioni hii. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu