Thursday, August 13, 2009

Kazi Ipo
Akiri kuwa na njama za ugaidi


DUSSELDORF

Mshukiwa mkuu wa ugaidi katika kile kinachoitwa "kesi ya Sauerland" Fritz Gelowicz amekiri makosa yake. Amesema yeye na wenzake watatu walikuwa na nia ya kuwaua askari wengi wa kimarekani waliyoko nchini Ujerumani kadri iwezekanavyo.

Mshukiwa wa pili anatarajiwa kuwasilisha ushahidi wake hii leo. Waendesha mashtaka wamesema kuwa watu wanne, wajerumani watatu na mturuki mmoja walipanga njama za kuyalipua majengo ya Marekani nchini Ujerumani kwa niaba ya kundi la kiislam liitwalo Jihad Union lenye uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaida.

Polisi waliwakamata watatu kati yao Septemba mwaka 2007 katika mkoa wa Sauerland.

No comments: