TANESCO Yatangaza Mgawo Wa Umeme Dar
Na Hussein Issa
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza mgao wa umeme katika jiji la Dar es Salaam kuanzia kesho hadi Agosti 28 mwaka huu.
Taarifa ya Tanesco iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari , ilisema mgao huo utakuwepo kutokana na kazi ya kufunga transfoma katika maeneo ya Masaki na Oysterbay.
Ilisema mgao huo utuzikumba sehemu nyingine kuanzia saa 1 asubuhi mpaka saa saba mchana , wakati sehemu nyingine zikikosa umeme kuanzia saa saba mchana mpaka saa moja asubuhi.
Sehemu zitakazokumbwa na mgao huo ni pamoja na Ubalozi wa Kenya, Japan, Urusi, India, Ufaransa na Iran, Heart Institute, STANBIC, barabara za Kenyatta, Kaunda, Kinondoni (sehemu), mtaa wa Laibon na Kwale na Kinondoni Hananasifu .
Zingine ni Golden Tulip, Coco beach, Barabara ya Tumbawe , Kajificheni , Josho la mbwa, sehemu ya Kenyatta , Oysterbay hospital, Ubalozi wa South Africa, Nigeria, Oysterbay hotel, International School of Tanganyika, Karibu Hotel, Barabara ya Hill na maeneo ya jirani.
Sehemu nyingine ni pamoja na maeneo ya Baobao sehemu ya Chole Kahama mining, Bandari quarters, Nasaco flats, ATC quarters, CCBRT hospital, TIRDO