Friday, June 19, 2009

MIGAGE

Enzi zetu miwa tulikuwa tunamenya kwa meno lakini siku hizi watu lazima wakatiwe vipande vidogo wanalia katika vifuko!!!

Aliyekuwa akiendesha mtandao wa ze utamu anaswa


Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.


Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.


Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.


Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.


Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania.Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani,ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.
Habari hii ipo hapa

Mlipuko kituo cha mafuta bamaga


Hivi kwa mfano haya matungi ya gesi yangelipuka hata sijui ingekuwaje kiukweli
Mchuma wa mafuta ulivyoteketea kwa moto kituoni hapo

Watu wakishuhudia mlipuko wa moto kituoni bamaga juzi asubuhi
Moto uliozuka jana saa 3:00 asubuhi katika kituo cha mafuta cha T.S.N. Bamaga kilichopo katika makutano ya barabara ya New Bagamoyo na Shekilango jijini Da es Salaam, unadaiwa kusababisha hasara kubwa.

Akizungumza baada ya tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Faruku Ahmed, alisema moto huo uliuunguza gari la kubeba mafuta aina ya Benz lenye tanki lake pamoja na jenereta ndogo.Hata hivyo kiasi kamili hakikutajwa, ingawa mwenye kituo alisema moto umesababisha hasara ya mamilioni ya Shilingi.

Moto huo ulidaiwa kusababishwa na hitilafu katika mashine ya jenereta iliyokuwa ikipampu mafuta kutoka kwenye kisima cha mafuta ya taa na kuhamishia katika gari kwa ajili ya kuyapeleka katika kituo kingine cha kampuni hiyo kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Mi nasema kama hii mitungi ya gesi ingefanya umbagala fulani sijui leo ingekuwaje ama wananchi wa jirani nao wangepatiwa fidia kama Mbagala?
Picha na habari kwa hisani ya Mzee wa Sumo

The Ngoma Africa Band wakiwasha moto! Hannover,Ujerumani

The Ngoma Africa Band aka FFU ! aka wazee wa kukaanga mbuyu wakiwasha moto wa kimataifa na mdundo wao toka bongo


Mr.Buti Jiwe aka Galinoma.Jr.Mwanamziki wa Kizazi kipya cha muziki wa dansi,anaefanyia kazi nchini Uholanzi,alialikwa na bendi ya Ngoma Africa akiwa kama Guest Artst,Pichani akiwajibika katika jukwaa la kimataifa la masala Festival,mjini Hannover,Ujerumani


Ras Makunja baada ya kumaliza kazi akiongea na mwanamziki Sefu Rengwe mwanamziki bingwa wa kupuliza vyombo vya kupuliza trumpe aka tarumbeta aka midomo ya bata,pia anaimba Sefu Rengwe ni mwanamziki aliyetamba sana na bendi ya The TATU NANE enzi zile.kwa sasa anaiongoza bendi ya Reggae ya SIX NATION, ambayo nayo irishiriki katika maonyesho ya masala.Kumbe bongo inautajili wa wanamziki

nani huyu?


Thursday, June 18, 2009

Tigo; " Express Yourself!"


Askari hao pichani ni maarufu kama ' Tigo'. Jina la moja ya mitandao maarufu hapa nchini. Na wana kibwagizo hicho cha ' Tigo Express Yourself' kwenye moja ya matangazo yao. Imeletwa na mdau wa http://www.kwanzajamii.com
kp na Busara zake !!
barabara za iringa kuwa tambarare karibuni
Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akipongezana na Balozi wa Denmark nchini,
Bjarne Sorensen baada ya kuweka jiwe la Msingi la ukarabati wa barabara ya TANZAM
sehemu ya Iyovi-Kitonga Gorge na Ikokoto –Iringa pamoja na barabra ya mchepuko ya
kuingia Iringa mjini zote zikiwa na urefu wa kilometa 149.6 katika sherehe
zilizofanyika Mazombe wilayani Kilolo Juni 14, 2009. Kulia ni Waziri wa
Miundombinu, Dr. Shukuru Kawambwa na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mohamed
Abdulaziz
LIBENEKE LA FACEBOOK KWA KIMATUMBI

Facebook Swahili version launched
The social-networking website Facebook has launched in Swahili, targeting more than 110m speakers of the language.A group of Swahili scholars launched the new version with the permission of the California-based internet firm.


Facebook use has spread over the past five years in East and Central Africa, where most Swahili-speakers live.

Analysts say a Hausa version could be launched next in West Africa and Zulu for southern Africa. Facebook already exists in Afrikaans.Symon Wanda, one of the project's initiators, said they wanted to launch a Swahili version to safeguard the future of the language

The youth, the future generation, if you look at the biggest percentage of users on Facebook, they are the youth," he told the BBC's Network Africa programme.

"They can easily navigate through when it's maybe a language they understand, which makes it easier to use the Swahili than to use the English.."

The BBC's Ruth Nesoba, in Nairobi, says the Swahili site has already been on trial for some time and word has spread quickly.Facebook's Simon Wanda says they have been monitoring the take-up and says more than 60% of Facebook users in East Africa are already using the Swahili version.

The bulk of Swahili-speakers live in Kenya, Tanzania, Uganda, eastern Democratic Republic of Congo, parts of the Horn of Africa, Malawi, Mozambique and the Indian Ocean islands.Facebook already exists in some 50 language versions.
kp leo
KUTANA NA ALBINO FULANI

BABU SIKARE A.K.A ALBINO FULANI

Babu Sikare si jina geni mjini Columbus Oh ni kijana machachari mwenye mbwembwe na ucheshi na kipaji kikubwa cha kughani na kutawala jukwaa ambacho kinajulikana na wachache, yeye ni mzaliwa wa Daressalaam nchini Tanzania.

Amezaliwa na ulemavu wa ngozi (Albino) lakini si wengi wanaotambua hali hiyo kwani wengine wanadhani yeye ni “mzungu” lakini hilo halimzuii kuonyesha cheche zake wala kufurahia maisha yake.

Babu Sikare aka Albino Fulani ameamua kupambana na mauaji ya Albino Tanzania akiwa amekulia Dar na kusoma Oysterbay Primary, anasema anakumbuka wenzake walikuwa wakitemea mate mashati yao ili wasigeuke Albino wakati alipokuwa shule ya msingi na kitu ambacho kamwe hatasahau ni kitendo kama hicho kufanywa na mwalimu wake!

Hivyo akiwa amehamia Marekani kiasi cha takriban miaka sita na nusu iliyopita kwa masomo ameguswa mno na hali ya mauaji nchini Tanzania na Burundi na hivi sasa anafanya juhudi za kupambana kuokoa maisha ya wenzake hao na ameamua kutoa single ya kwanza iitwayo “Barua kwa Mama” hii ni kisa cha kweli baada ya kumpoteza mama yake mzazi hayati Grace Mwasi Sikare.

Albam yake kamili bado iko jikoni inapikwa hapa Marekani na anashirikiana na wanamuziki kama vile Mkali Fulani, Mtaalam Fulani, Chid Benz na Tinted pamoja na mambo mengine ya maisha ya kila siku album hii itaelezea maisha ya Albino kuwa ni sawa na watu wengine wa kawaida.

Single yake hiyo itazinduliwa Columbus Oh 20/06/09 katika ukumbi wa Boomerang. Wadau wa Columbus, Indiana, Michigan na vitongoji vyake mnakaribishwa sana.

Wakazi wa Dar na vitongoji vyake wajiandae kwani Babu Sikare anategemea kutoa albamu yake Tanzania mwezi Julai ambayo itakuwa na nyimbo 9 na itakwenda kwa jina hilo hilo la kwake “Albino Fulani”.


unazikumbuka nguzo tano za ujamaa??

Dear Wadau,
I know some of you might say 'zimepitwa na wakati' but if you read between the lines, they are somehow relevant.
Mdau Lilly
----------------------------------------

Katika kipindi hiki ambapo jamii mbalimbali duniani zinapigania haki na usawa hasa ule wa kumiliki rasilimali ambazo zimepokwa na zinazidi kunyakuliwa na waumini wa itikidi ya uliberali mamboleo ni vyema tukajikumbusha Nguzo Tano za Ujamaa hasa nguzo ya nne inayogusia rasilimali kuu ya ardhi:

NGUZO TANO ZA UJAMAA - KWA MUJIBU WA JULIUS K. NYERERE, SABA SABA 1970

1. 'WATU WOTE NI SAWA'"...

Kama hukubali hilo, yaani kama unadhani watu wengine ni miungu wengine, malaika, wengine nusu-nyani, basi hukubali ujamaa. Ujamaa kwako hauna maana, kwa sababu ujamaa unahusu usawa wa watu: hapo ndipo unapoanza...Sisemi usawa wa urefu wala ufupi; kwa urefu namzidi Kawawa, sana tena. Sisemi maguvu, hata; nasema utu, watu, na ubinadamu wao. Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe? Kama huliamini hilo, utakuwa mjamaa? Hilo la kwanza... mkaliulize-ulize, mlielewe maana yake. Na mtu anayepinga ujamaa naye ajiulize kama anapinga hilo nalo. Mtu mpingaji ujamaa aseme, 'Hilo nalo, usawa wa watu, napinga; kwamba binadamu wote hivi si sawa'" - Mwalimu Julius K. Nyerere

2. 'LAZIMA MTU AFANYE KAZI'

"...Binadamu hao unaotuona hapa, na hao waliosambaa dunia nzima wanaishi kwa kazi. Hawana namna nyingine ya kuishi. Wakiacha kufanya kazi watakufa; hawana namna nyingine; kuishi kwao, na kuendelea kuishi, lazima wafanye kazi...Lakini binadamu haishi kama farasi. Binadamu haridhiki kuishi kama farasi au punda; binadamu ana kitu anakiita maendeleo; lazima aendelee...Wakati mwingine ili kusudi maendeleo haya yaje wana shughuli za kupigana misasa akili, wanapanuana mawazo tu, nayo ni kazi...nendeni mkaulizane...kama kazi si kitu cha lazima, kama binadamu anaweza kujikalia tu hafanyi kazi, akaishi, na maendeleo yakaja bila kazi. Na huyo anayepinga ujamaa naye ajiulize kama hilo analipinga? Na hilo la kufanya kazi analipinga au kuna jingine analopinga?" - Julius K. Nyerere

3. 'HAKUNA MTU KUMNYONYA MTU'"...

Kama binadamu ni sawa, tunalikubali hilo...Pili tunasema kitu kazi ni jambo la lazima kwa kila mtu, hakuna aliyesamehewa kazi. Basi siwezi kukufanyia kazi. Kukufanyia kazi maana yake ni kwamba wewe unasamehewa kazi! Siwezi kukufanyia kazi. Wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya. Sio mimi nifanye, wewe hufanyi; lazima ufanye kazi. Kwa hiyo wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya kazi; kila mtu atafanya kazi. Yaani namna ya kulitamka hilo ni kwamba kunyonyana hakuna. Hakuna mtu kumnyonya mtu; sasa tena msingi wa kumnyonya unatoka wapi? Tumesema watu sawa; na mtu ili aishi hana budi afanye kazi, na kazi ndio msingi wa maendeleo. Sasa mwanachama... ajiulize kama anaweza kuwa mjamaa na huku ananyonya! Unamnyonya mkeo; mkeo anakwenda kufanya kazi wewe unakwenda kupiga chibuku; hivi kweli mjamaa wewe? Tunasema kazi jambo la lazima, lakini wewe hufanyi kazi, unamnyonya mkeo. Wewe mjamaa? Nasema na hilo mjiulize...Unaweza kuwa mjamaa na huku unanyonya? Na anayepinga ujamaa ajiulize hilo nalo analipinga, kwamba yeye anaona kunyonya ni sawa tu! Sawa yeye kunyonya mwingine au wengine kumnyonya yeye, huyu anayesema kunyonya ni sawa. Kama kunyonya ni sawa baba, sasa tuanze kunyonya, au mkuki kwa nguruwe?" - Julius K. Nyerere


4. 'VYOMBO MUHIMU VIMILIKIWE PAMOJA'


"...Kama watu ni sawa; binadamu wote ni sawa; kazi ni jambo la lazima kabisa; kunyonya ni haramu; la nne linafuata: Vyombo vyote vya lazima, vinavyohitajika kwa maisha ya binadamu kwa kufanyia kazi lazima vimilikiwe kwa jumla. Ardhi lazima imilikiwe kwa jumla maana tusipoimiliki ardhi kwa jumla tutamwachia Rashidi Kawawa na Sheikh Karume wao wawe ndio wenye ardhi, na ardhi ni kitu cha lazima kwa maisha, hebu tuone kwanza usawa utakuwaje. Itakuwa lazima twende kwa Rashidi na kwa Karume, 'tafadhali bwana nataka ardhi'. Umekwishamwita 'Bwana' huyu; usawa umekwisha. Lakini vilevile kama Sheikh Kawawa ana ardhi, na Sheikh Karume ana ardhi, hawa hawalazimiki kufanya kazi. Kwa nini wafanye kazi? Hawawezi kufanya kazi. Tumesema kazi ni kitu cha lazima kwa kila mtu, lakini hawa hawawezi kufanya kazi, watakaa tu wanatutoza kodi kwa ardhi yao. Ndiyo wanatunyonya hivyo tena. Mimi nafanya kazi; mimi nalima. Halafu Rashidi anasema, 'Ukishalima mahindi ukapata magunia matano, moja langu'. Ndio ananyonya hivyo. Anavunja kanuni ya usawa; anavunja kanuni ya kazi; anavunja kanuni ya kutonyonya. Kwa nini? Kwa sababu tumemruhusu amiliki yeye vitu ambavyo vinastahili viwe vya wote. Mtu ambaye yeye ana ardhi; umemkabidhi viwanda, ukishakuwa umemkabidhi majambo mengine haya, umemwongezea nguvu zake, yeye utu wake umeongezeka-ongezeka na wangu mimi umeupunguza-punguza. Kwa hiyo vitu vilivyo vya lazima kwa kila mtu, kama ardhi ambayo ni ya lazima kwa kila mtu, lazima vimilikiwe na wote. Sasa...mjiulize kama unaweza kuwa mjamaa kweli huku unajidai ardhi yangu? Na wanaopinga wanatakaje? Hao wanaosema ujamaa mbaya. 'Eti vitu vyote viwe vya ujumla'; wengine waongo, 'Eti wanasema hata wakina mama wawe wa jumla'. Tunasema ardhi, hatusemi kina mama, tunasema ardhi viwanda, madini: kwa nini mtu mmoja anakwenda kuvinyakua vikawa vyake hivi!" - Julius K. Nyerere


5. 'KUUNDA NCHI BILA MATABAKA'

"..Kama tunakubali kuwa watu wote ni sawa; na watu wote ni lazima wafanye kazi, mtu asimnyonye mtu; na mali, mali kubwa, sikusema shati langu liwe la Rashidi: misingi ya uchumi kama mabasi yale yanapita iwe kwamba tunasema mabasi yetu, asiweko mheshimiwa mmoja pale anasema 'Basi langu lile!' Basi lako! Yupo dereva mle anaendesha, anasema dereva wake! 'Dereva wangu' - dereva wako, wewe unaweza kuwa na dereva? Dereva anaweza kuwa dereva wa umma, sio dereva wako. Dereva ni sawa sawa na mwalimu; mwalimu wa umma, daktari wa umma, dereva wa umma. Huyu anakuwaje 'wako'? Hata askari siku moja utasema wako. Kama tunakubali watu wote ni sawa; watu wote lazima wafanye kazi, hakuna kunyonyana; mali,vitu vyote vile vya jumla lazima viwe vya umma; maana yake ndio kusema tunataka kuunda nchi ambayo haina tabaka: hakuna mabwana na watwana." - Julius K. NyerereNUKUU ZIMETOKA KWENYE UJAMAA NI IMANI: MOYO KABLA YA SILAHA, 1973: EAPH
VODACOM KUMPATA MILIONEA ATAKAYEJIZOLEA TSH 100 MILIONI LEO
Vodacom Tanzania leo itampata milionea wake atakayejizolea Tsh 100 Milioni pesa taslimu katika droo kubwa itayorushwa moja kwa moja (LIVE) na kituo cha TBC1 kuanzia saa 3 usiku.
Mnamo mwezi Machi mwaka jana wa 2008, Vodacom Tanzania ilizindua promosheni ambayo kupitia zawadi zake zilizokuwa zinawagusa watu wengi, iliweza kutimiza malengo ya wateja wake.
Promosheni hii ilijulikana kama TUZO DROO iliyodumu mpaka mwezi Machi mwaka huu. Zawadi nzuri za kila wiki kama vile washindi 100 kupata muda wa maongezi wenye thamani ya Tsh 50,000 kila Mmoja pamoja na washindi 7 kujinyakulia Tsh 1 Milioni kila Mmoja.
Vilevile kulikuwa na zawadi za kila mwezi ambapo mshindi 1 aliweza kujizolea kitita cha Tsh 40 Milioni kila mwezi. Na mnamo mwezi Aprili mwaka huu, Vodacom ilizindua promosheni nyingine ikiwa ni mwendelezo wa promosheni ya TUZO DROO.
Promosheni hii ilijulikana kama TUZO MILIONEA ikiwa na zawadi ya muda wa maongezi wa Tsh 100,000 kwa mshindi mmoja kila siku. Promosheni hii ilikwisha Jumapili tarehe 14 Juni saa 5.59 usiku.
Vilevile, Vodacom iliweza kutangaza rasmi zawadi kubwa kabisa ya Tsh 100 Milioni itakayokwenda kwa mshindi Mmoja kwenye droo itakayochezeshwa leo hii usiku. Usikose kuwa mbele ya luninga yako kuanzia saa 3 usiku kwenye kituo chako bora cha TBC1 au DSTV chaneli 143 na ushuhudie ni nani atakayeibuka mshindi wa Tsh 100 Milioni pesa taslimu!!
clouds 88.4FM wajitolea damu
kikosi cha wafanyakazi wa clouds 88.4 FM kilichojitolea damu mwishoni mwa wiki dar katika siku ya kuchangia damu duniani ambapo waandaji wa shughuli hiyo wamekishukuru sana kituo hicho kwa kujitolea damu pamoja na kupromoti vilivyo siku hii
mambo ya ahmed viryala

Sunday, June 14, 2009

mazishi ya mzee john kolos kapinga
Mke wa rais mama Salma Kikwete akiweka shada la maua juu ya kaburi la ndugu John Kolos Kapinga wakati wa mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa SUKITA ndugu John Kolos Kapinga yaliyofanyika nyumbani kwake eneo la Kimara stop over jijini Dar
Mama Revy Kapinga akiweka shada la maua juu ya kaburi la mumewe marehemu John Kolos Kapinga wakati wa mazishi yaliyofanyika jana jioni eneo la Kimara stop over jijini Dar
Mke wa marehemu John Kapinga akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe marehemu Kapinga wakati wa mazishi yaliyofanyika jana jioni eneo la Kimara stop over jijini Dar
Mapadre wa kanisa Katoliki Parokia ya Mavurunza wakiongozwa na Paroko wa kanisa hilo Erasto Nyoni wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu John Kolos Kapinga.Marehemu Kapinga alizikwa jana jioni nyumbani kwake eneo la Kimara stop over, Dar es salaam
Ndugu , jamaa na watoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa SUKITA marehemu John Kolos Kapinga wakiwa mbele ya kaburi la John Kapinga wakiongozwa na mke wa marehemu mama Revy Kapinga (wa pili kulia mstari wa mbele). Picha zote na mdau Aaron Msigwa wa Maelezo



libeneke jimboni vunjo
Wanakijiji wa kijiji cha Singi'si wilayani Arumeru wakibomoa nakuchukua mali za mmiliki wa shamba ambalo wanadai ni mali ya kijiji hicho na kufanya uhalifu mkubwa katika shamba hilo linadaiwa ni la mh. mbunge wa Vunjo mheshimiwa Kimaro.

hapa ni kama wamelifanyia plunning shamba la migomba ambalo liliangamizwa lote na wakaondoka na mikungu ya ndizi.pia katika vulugu hizo askari mmoja alijeruhiwa na kunyang'anywa bunduki ambayo hadi hivi sasa haijapatikana ila wahalifu wapo rumande kuisaidia polisi pia raia mmoja aliuawa katika vurugu hizo.

Mdau wa Vunjo
zawadi ingine toka kwa baraka chibiriti
video
baada ya kutoa watu machozi kwa video ya awali ya hawa vijana wa shule ya msingi kule same, mdau baraka wa chibiriti aliyeko Cesena, Italy, anasema kafurahishwa sana na jinis wadau mlivyofurahishwa na video hiyo. na leo kaamua kutupa ingine
vodacom foundation yamwaga misaada mafia
Meneja Uhusiano wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akikabidhi mabati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Lewis Kalinjuna kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Kitomondo, wilayani humo.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Lewis Kalinjuna kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara ya shule ya Kitomondo.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kulia) akikabidhi kemikali kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kitomondo, kwa ajili ya kusaidia mafunzo kwa njia ya vitendo katika maabara ya shule hiyo, wilayani Mafia.



hajra badru atamba miss mwanza

Mrembo Hajira Badru ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) alishiriki mashindano ya miss mwanza yaliyofanyika uwanja wa ccm kirumba na kutamba hadi kuchukua nafasi ya sita. Mrembo mwingine ambaye pia albino, Grace, alijitoa baada ya kukabiliwa na shinikizo la masomo chuoni SAUT
Mrembo huyo alishangiliwa na umati wa watu kila alipojitokeza jukwaani katika mavazi mbalimbali kama picha zinavyonyesha. Habari kamili na picha zaidi tembelea www.florasalon.blogspot.com
hajra badru atamba miss mwanza

Mrembo Hajira Badru ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) alishiriki mashindano ya miss mwanza yaliyofanyika uwanja wa ccm kirumba na kutamba hadi kuchukua nafasi ya sita. Mrembo mwingine ambaye pia albino, Grace, alijitoa baada ya kukabiliwa na shinikizo la masomo chuoni SAUT
Mrembo huyo alishangiliwa na umati wa watu kila alipojitokeza jukwaani katika mavazi mbalimbali kama picha zinavyonyesha. Habari kamili na picha zaidi tembelea www.florasalon.blogspot.com

Monday, June 8, 2009

Being simple doesn’t cost a thing!














Wazee wetu Afrika wanaweza kuwa simple kama hivi, ama ni blessing from above?
usia wa baba wa taifa
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
MKUU WA NANIHII....
NAOMBA NIPE LAU NAFASI NIPATE SEMA KIDOGO JUU YA BABA WA TAIFA AMBAYE TUTAKE TUSITAKE ALIKUWA ANAONA MBALI KULIKO INAVYODHANIWA. NAOMBA UWEKE NUKUU YAKE HII KATIKA WAKATI HUU ILI WADAU WACHANGANUE NA KUCHANGIA BILA KUHARIBU HALI YA HEWA.
"DOLA LAZIMA ISIMAMIE SHERIA ILI KULINDA HAKI NA KUHIFADHI AMANI. WAJIBU HUU USIPOZINGATIWA, WATAIBUKA MANABII WENYE KUIHUBIRI HAKI KWA KUWAHUKUMU WENGINE. HAMTABAKI SALAMA MKIFIKIA HAPO"
-J.K. NYERERE
mwamvita na watoto yatima kijiji cha SOS
Mkuu wa Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba (kushoto) akisalimiana na watoto wa kituo cha kulea watoto cha SoS Children's Village, walipotembelea katika kituo hicho jijini Dar