Monday, February 16, 2009

SANGOMA KUKIONA MZA




Waganga waanza kufanyiziwa kuokoa maalbino
AGIZO la Waziri Mkuu alilotoa wakati wa ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa kuhusiana na ukomeshaji wa mauaji ya albino, limeanza kutekelezwa baada ya vibanda 17 vya nyasi mali ya waganga wa jadi kubomolewa wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Zoezi hilo la ubomoaji ambalo limefanyika kwa mgambo wa jiji la Mwanza katika zoezi lililosimamiwa na viongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza chini ya mkurugenzi wake Willson Kabwe.
Vibanda vya nyasi vilivyobomolewa ni 13 pamoja na nyumba nne za nyasi ambazo ni mali ya mganga Masai Kasanga aliyekuwa amejenga jirani na shule ya sekondari ya Lumala iliyopo wilayani Ilemela jijini Mwanza. Akielezea zoezi hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Willson Kabwe, alisema mamlaka yake imeamua kutekeleza agizo hilo la serikali ambalo lilitolewa na maelekezo yaliyotolea na mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. James Msekela katika hotuba yake wakati wa kupokea maandamano ya maalbino jijini Mwanza.
“Zoezi la leo ni utekelezaji wa agizo la serikali, na hili litakuwa ni zoezi la kudumu kwa vile ujengaji wa vibanda hivi unapingana na sheria ya mipango miji ambayo inazuia kuwepo kwa vibanda katika maeneo ya taasisi ama makazi ya watu. Litakuwa endelevu na leo tumeanzia hapa Ilemela”Alisema Kabwe.
Alisema kabala ya kumvunjia mganga huyu alipewa taarifa ya kuhama na kubomoa vibanda vyake ikiwa ni pamoja na kulipwa fidia ya ardhi ya eneo hilo sh. 1.2 milioni ambalo alikuwa akilimiliki kihalali lakini licha ya kupokea fidia hiyo aligoma kuhama hatua ambayo imelifanya jiji kuchukua hatua hiyo.
Akielezea hatua hiyo mganga huyo Masai Kasanga ambaye ni mwenyeji wa Bukumbi wilayani Misungwi alisema hakuweza kuhama licha ya kutakiwa kufanya hivyo na kulipwa fidia kutokana na ukweli kuwa fidia hiyo ni ndogo na kwamba uongozi wa jiji haukumpa fidia ya kuhamisha mali zake pamoja na wagonjwa wake.
“Nilipokea fidia lakini niliwaeleza kuwa wanapaswa kunipatia na fedha ya kuhamisha wagonjwa wangu pamoja na vitu vyangu hawakunipa ndiyo maana sikuhama, lakini sasa wamefanya hivi, basi” alieleza.

DOGO AULA KWA PINDA




Mtoto George Bush wa Chato ambaye amechukuliwa na familia ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa ajili ya kumlea maisha yake yote mpaka atakapojitegemea! Dogo ameahsanza kutanua na mzee katika ziara! Big Up Mzee Pinda, Upendo wa hali ya juu!

Thursday, January 29, 2009

Ama kweli duniani kuna mambo.!


mkubwa fella aja na singo yake kuleta heshima


Anaitwa Said Fella lakini unaweza ukaanza kumuita kwa jila la Mkubwa Fella nae bila hiyana huitika kwa bashasha kabisa.Kwa wale wasiomfahamu vyema ni yule meneja wa kundi la Wanaume TMK Familly lenye makao yake makuu kule kule Temeke jijini Dar.

Mkubwa Fella amenitonya hivi punde kwa njia ya simu kwamba ameingia studio ya Sound Crafterz kwa ajili ya kurekodi singo yake ya kwanza itakayoitwa 2009.Amesema kuwa anataka kuwaonesha baadhi wasanii ambao wamekuwa wakimfuata wakati wa shida na kusaidiwa, wakishiba wanakuja na maneno ya kashfa na kiburi kama baadhi ya wasanii wengine ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa maneno ya hapa na pale.

"Nataka kuwaonesha baadhi wasanii kuwa hata mimi na naweza,ili kuthibitisha hilo wakae mkao wa kula nakuja na singo yangu ya kwanza itakayoitwa 2009, sasa nipo studio ya Sound Cfafters kwa ajili kurekodi hiyo singo,ambayo anaamini itawashtua wengi,kwamba aalahh hata Mkubwa Fella anaweza"alibainisha Mkubwa Fella

bongo mvua kiduuchu mtafutano


Bongo bwana mvua kiduuchu tu balaa kila mahali,Mvua ya kiasi imenyesha leo asubuhi jijini Dar,lakini adha ya msongamano wa magari na mifereji ya maji machafu kujaa imekuwa kero kubwa sana

nakuja na mambo mapya-Steve Nyerere


Steve Nyerere akiwa kwenye maandalizi makubwa ya kipindi chake ambacho kitahusisha mchakato mzima unaoizunguka jamii pamoja na wageni waalikwa ambao watakuwa wakichangia mada hizo kwa namna moja ama nyingine

Shoto ni Boss wa HATMAN PRODUCTIONS pamoja na mwanamuziki wa FM Academia Patchou Mwamba wakivutiwa na uandaaji wa kipindi cha Steve Nyerere talk show kitakachoanza kurushwa hewani mwezi ujao na televisheni ya TBC 1 jijini Dar

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini maandalizi makubwa ya kipindi cha Steve Nyerere talk show

Steve akimuigiza Rais Jakaya Kikwete wakati wa maandalizi ya kipindi chake

Msanii mchekeshaji na muigizaji wa sauti mbalimbali za watu maarufu ajulikanae kwa jina la Steve Nyerere akimuigiza Rais JK katika moja ya hotuba zake,hayo ni moja ya maandalizi makubwa na ya kufa mtu ya utengenezaji wa kipindi chake kitakachoitwa Steve Nyerere Talk Show kitakachokuwa kinarushwa na televisheni ya TBC hapa jijini Dar.Kipindi hicho kinachorekodiwa na kampuni ya HATMAN PRODUCTIONS kinatarajiwa kuanza kurushwa hewani mwezi ujao,haya wadau kaeni mkao wa kula mambo mapya yanakuja TBC.

NB: Ukimuhitaji Steve Nyerere katika shughuli zako mbalimbali wala usisite bofya namba hii 0715 782424 na utasikilizwa na kujibiwa haraka.

Askari wa JWTZ amuogesha dereva wa school bus



Hiyo picha nimetumiwa na mdau, naomba tuiwakilishe hivyo
hivyo japo haionekani vizuri:-

"Kaka naomba uiwakilishe hii picha ya askari wa JWTZ aliyemuogesha
dereva wa school bus pale kawe darajani kwa komba asubuhi ya leo baada
ya kumwagia maji viatu vyake ambavyo anadai alivipiga kiwi leo asubuhi.
Haya sio ya kusikia nimeyaona kwa macho na watu wadau wengine pia
alishuhudia. Hebu tuulize wana jamii; Mlinzi wa wananchi anapofanya kitu
hii wewe unapata picha gani?" Nawakilisha

NB:Wadau mimi kama kawaida yangu ya ujumbe,si mnajua mjumbe hauwawigi

kp na Busara zake !!

kikwangua anga cha kampuni ya nanihiii


Kikwangua anga kingine cha kampuni ya nanihii kikapandishwa taraatibu,ebwanaee bongo imecharuka kwa vikwangua anga si mchezo

Wednesday, January 28, 2009

bongo kutamu
maeneo ya mwanga


Blaza Kadidi, na mwenzio Kamanda Kombe

Nimekutumia hii picha niliyoipiga hivi punde, ili na wadau wengine wajionee Bongo isivyo tambarare.

Ni wiki mbili tu zimepita tangu ajali itokee huko Tanga kwa basi kuligonga nyuma lori lililokuwa limeharibika, pasi kuwa na vielelezo vyovyote kuwa limesimama kwa ubovu, na wala hapakuwa na reflectors nyuma ya lori hilo.

Hebu tazama hili gari ya takataka, hapa niliibamba ikikata kona, kutoka barabara ya M/nyamala kuingia Kawawa, indiketa zake hazifanyi kazi, taa za nyuma hata moja haiwaki, kibao cha namba hakipo, na huu wavu waliozuia nao uchafu unavujisha kidogo kidogo, thus uchafu ulikuw aunadondoka barabarani. Pia tairi zake kipara wakati limebeba mzigo mzito namna hii.

Swali; Hii inamaanisha traffic hawalioni? Au mnaliona na huwenda hawaruhusiwi kulikamata? au huwenda ndio linavyotakiwa kuwa kiuchafuuchafu?, au hili lori liue watanzania wangapi ndio mpate pa kuanzia kuchukua hatua ili tuione mnafachapa kazi?

Imagine gari kama hilo mdau linapata breakdown usiku, alafu unakuja nyuma yake itakuwaje? Natumai kama mhishimiwa fulani angekuwa na maono kuwa baada ya siku kadhaa gari yake ingejibamiza hapo nyuma ya hii lori, maamuzi yake ya leo yangekuwa tofauti.Au angekuwa na maono kuwa school bus alilopanda mtoto wake italivaa lori hili kwa nyuma, angechukua hatua flani leo. Kwakuwa haya yoote hatuwezi kuwajua ni bora kuchukua hatua leo.

Mdau MG
( Koplo wa polisi jamii)