Thursday, March 5, 2009

wema atoka rumande kwa dhamana leo
mrembo wema sepetu akipewa pole na rafiki yake baada ya kuachiwa kwa dhamana leo mahakamani kinondoni anakikabiliwa na shtaka la kuharibu gari la mwigizaji steve kanumba. mrembo huyu aliyepata kuwa miss tz alikuwa rumande toka wiki iliyopita baada ya kukosa dhamana alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
mama mzazi wa wema sepetu akisaidiwa na nduguye wa kiume ilibidi watumie nguvu wema aondoke nao wao na sio rafikiye ambaye alifika hapo mahakamani















Taifa stars wameremeta
taifa stars wakiwa wamekula pamba zao mara waliporejea toka ivory coast Jana
kp na busara zake.


karibu afande!
JK akikaribishwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange kuzindua kamandi ya jeshi la ardhini katika kambi ya Nyerere ameneo ya Msigani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo. Kulia ni Meja Jenerali Wynjones Kisamba ambaye ndiye kamanda wa kamandi hiyo

Wednesday, March 4, 2009

taifa stars yatua dar leo
beki wa taifa stars shardack nsajigwa akiongea mara tu baada ya kutua dar leo0 wakitokea ivory coast
kiongozi wa msafara waziri wa nchi ofisi ya maikamu wa rais mh. muhammas seif khatibu akiongea mara bazada ya taifa stars kutua leo dar

kocha marci maximo akiongea na katibu mkuu wa tff frederick lameck lugano mwakalebela

ujumbe toka kwa ndugu zetu albino
Afisa Habari wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania,wa pili kutoka kushoto Matina Nkurlu akiwa na walemavu wa ngozi(Albino)wakionyesha ujumbe wao kwa jamii ya kitanzania kwa kutumia mabango katika viwanja vya chuo cha ushirika Moshi wakati wa mbio za kili marathoni mwishoni mwa wiki. Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidia walemavu wa ngozi kwa misaada mbalimbali
mjadala wa kocha marcio maximo; abaki ama aondoke?
kocha wa taifa stars marcio maximo toka brazil akiwa na wakongwe wa soka ambao toka shoto ni kipa james kisaka, kipa juma pondamali na beki athumani chama.
kwa heshima na taadhima globu ya yamii inaanzisha mjadala wa kumjadili kocha maximo kwa nia ya kupata mawazo ya wengi baada ya kutolewa katika michuano ya CHAN kule ivory coast majuzi ambayo ndiyo ilikuwa ni kipimo tosha cha uwezo wake katika muda wa miaka miwili ya mkataba wake.
1. je, maximo amefanya kile alichokuja kukifanya?
2. mwezi julai mkataba wake unamalizika, je aongezewe ama aondoke?
3. kuna haja ya kuwa na kocha wa nje ama tubaki na wazalendo?

wakati ni kweli globu ya inawezekana inakaribisha maoni ya aina yoyote kuhusiana na mstakabali wa maendeleo ya soka nchini, si uwongo kwamba maoni yatayochafua hali ya hewa hayafai na hayatoona mwanga wa jua. hivyo mdau unaombwa utoe maoni bila jazba ama kashfa ili tujenge badala ya kubomoa.

-Kadidi2


kocha wa vijana afungasha virago
kocha wa timu ya taifa ya vijana kutoka brazil marcus tinocco (pichani akikagua timu ya vijana wakati wa copa coca cola mwaka jana, dar) ameliandikia shirikisho la soka nchini (TFF) barua ya kujiuzuru nafasi hiyo kwani amepata kibarua kipya huko trinidad and tobago kufundisha timu ya daraja la pili ya huko.
globu ya jamii imethibitisha kwamba tinocco aliitoa barua hiyo hata kabla ya taifa stars kwenda ivory coast kwenye michuano ya CHAN, ambapo ndiyo kusema hatuna tena kocha mtaalamu wa timu ya taifa ya vijana.
bongo star search tanga 2009
wadau kibao walijitokeza katika msako wa bongo star search tanga wikiendi hii
hawa ndio washindi wanne wa tanga wa BSS

Vodacom Tanzania pamoja na uongozi mzima wa Bongo Star Search 2009 tunawashukuru wale wote waliojitokeza kujiandikisha na kufanya usaili pale Tanga na tunawatakia kila la kheri kwa wale washindi wane waliofuzu mchujo. Wakazi na wale wote wenye vipaji vya uimbaji kaeni tayari kwani sasa Vodacom Tanzania inahamishia kinyang’anyiro cha Bongo Star Search 2009 mjini Kigoma tarehe 7 na 8 Machi 2009.

msiba ITV: Rehema Mwakangale hatunaye tena
Mtangazaji wa ITV Rehema Mwakangale (kulia) ametutoka jana asubuhi katika hospital ya Mikocheni alikokuwa amelazwa. Kwa Mujibu wa taarifa kupitia Radio One, mipango ya mazishi itakuwa kwa bibi yake Sinza karibu na Deluxe bar. Mola ailaze roho ya marehemu peponi
AMINA
Pichani ni marehemu Rehema Mwakangale akimhoji mama wa mtoto Samuel Nkya aliyeharibika sura na kupelekwa India kwa matibabu. Rehema alikuwa mstari wa mbele kufuatilia matibabu ya mtoto huyo ambapo globu ya jamii ikishirikiana na ITV viliweza kuchangisha pesa kufanikisha hayo matibabu. Picha zaidi BOFYA HAPA