Tuesday, January 27, 2009

Watoto wa mitaani ni tatizo kichizi dom

Kijana aishie katika mazingira magumu akiwa amelala katika bustani ya Nyerere mjini Dodoma. Idadi ya watoto kama hawa inazidi kuongezeka mkoani Dodoma ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kuna zaidi ya watoto elfu 14 wanaoishi katika mazingira magumu mkoani humu, ambapo asilimia 62 ya idadi hiyo bado wapo mitaani.

Wednesday, January 21, 2009



RTO-IRINGA ISIWE NGUVU YA SODA

Mhariri,

NAFURAHI kusema kwamba nimefurahishwa na RTO-Iringa bwana Mnubi ambaye kama sijakosea ni senior superitendant kicheo.Bwana huyu juzi tarehe 19/01/ 09 alitusimamisha pale Iringa{check point} na kuanza kukagua magari yote yanayosafiri mikoa ya jirani kupitia mkoa wake.Akishirikiana na vijana wake pamoja na mkaguzi wa magari wa polisi wa mkoa,walikagua kama kila gari lina dereva wa ziada pia kama linakidhi mahitaji ya kusafiri safari ndefu,kwa magari ambayo hayakukidhi sheria hizo yalitozwa faini ya shilingi laki moja kama faini au kumwacha kondakta apelekwe kortini na wengine kuruhusiwa kuendelea na safari.

Kwa kitendo hicho kililaaniwa na abiria wengi wakiwemo wa basi nililokuamo HOOD la Tunduma wakidai kwamba wanacheleweshwa bila kujua kwamba RTO na timu yake wako kazini pia wako pale pia kulinda haki ya abiria na kupunguza ajali barabarani cha kushangaza ni kwamba abiria wa basi langu na mabasi mengine walianza kumzomea na kumtukana RTO wakisahau haki yao ya kufika salama,ni muhimu madereva kupokezana hasa kwa safari ndefu kwani siyo nzuri kiafya pia umakini barabarani unapungua kwa sababu akiwa mmoja anachoka.

Binafsi naunga mkono kazi ya RTO-Iringa ila TU ISIWE NGUVU YA SODA.Kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza ajali barabarani natoa rai abiria tusiwe tunatetea upumbavu unaofanywa na madereva kama waliofanya basi nililokuamo na mengine.Pia vita ya kupunguza ajali si ya askari polisi tu bali na abiria pia kwani wao ndiyo walengwa wakuu.

Hii iwe changamoto kwa ma RTO wengine kwani kutokua kwao makini kunawapa kiburi madereva na madereva wanamwona RTO –Iringa mnoko wakati yuko kazini.Chakushangaza tulitoka Dar,Pwani na Morogoro lakini hatukukaguliwa hii inanipa picha ya UZEMBE wa ma RTO wa mikoa hiyo.Hivyo pongezi kwa RTO-Iringa na timu yake, pia Iringa iwe ni mfano ,

kwani mabasi hubeba roho za watu na si mawe.

Kasuga (mzee wa muliko),


Tuesday, January 20, 2009

Tunakukumbuka Bibi Yetu
Delphina Kasuga .

Bibi yetu Delphina Kasuga kesho tarehe 21/01/2009 tutakuwa tunafikisha mwaka wa tatu tangu ututoke katika ulimwengu huu pale hospitali ya Mama Ngoma ilikuwa ghafla sana ingawa tulikupenda sana ila Mungu alikupenda zaidi.
Wajukuu zako tunakukumbuka sana Ronald Kasuga, Fina Kasuga ,Joshua Kasuga, Rose Lema, Ferald Akyoo, Magdalena Akyoo, Safari Kawa, Agustino Kasuga, Babu na wengineo wengi neo wengi ulioshirikia na nao kwa ukaribu .
Tutakukumbuka Daima .
Raha ya milele umpe Ee Bwana na mwanga wa milele Umwangazie Astarehe kwa Amani Amina .

Monday, January 19, 2009


Baada ya ziara za mikoani na kumwaga sumu katika Operesheni Sangara sasa Viongozi wa Chadema wameingia jijini Dar es Salaam kuendeleza operesheni hiyo.
tarehe 12 ndio walitanagaza rasmi kuvunja ndoa na vyama vingine vya upinzani!!
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema wamegundua kuwa kuna vyama vingine ambavyo ni mamluki katika upinzani na hivyo Chadema kitapambana chenyewe kuwakomboa waTz ila jamani kuna ya ccm inaitwa nyavu kama sikosei kwa hiyo hapo ni raha tupu hiyo wameizindua kutoka Arusha .
Mlimani Mambo
Magumu....
JESHI la polisi limelazimika kuvunja maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,yaliyokuwa yameandaliwa na serikali ya wanafunzi iliyoripotiwa kutotambuliwa chuoni hapo (DARUSO).Maandamano hayo yaliandaliwa kwa lengo la kupinga utaratibu wa udahili unaoendelea kwa kuwarudisha wanafunzi ambao wamekamilisha malipo yao yote.Mwananchi ilishuhudia wanafunzi wakiwa nje ya chuo wakijiandaa kuandamana huku wakiwa wameshika mabango yanayochochea maandamano, huku wengine wakiwa wanaendelea na udahili kama kawaida.
"Tumeamua kuandamana leo uongozi uone wenyewe kwamba unachokifanya sio halali kwani kumrudisha kuendelea na masomo mwanafunzi mwenye uwezo na kumuacha asiye na uwezo ni sawa na ukandamizaji,"walisikika wanafunzi hao wakiwa wameshikilia mabango tayari kwa maandaamano."Habari ya Hussein Issa na Picha ya Emmanuel Herman.
Mramba ruksa kuhudhuria vikao vya Bunge
Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba, ameruhusiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kuhudhuria Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. Hata hivyo, mahakama hiyo imesema inaweza kumwita wakati wowote itakapomhitaji kwa sababu mbalimbali zinazoweza kujitokeza. Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Hezron Mwankenja, alisema jana kuwa ametoa uamuzi huo baada ya kusoma vifungu mbalimbali vya Katiba na kuona hakuna sababu ya kumzuia. ``Lakini tufahamu kuwa ruhusa hii, haizuii mahakama kumwita wakati wowote itakapomhitaji hata kabla ya tarehe ya kusikiliza kesi yake ambayo ni Februari 2 mwaka huu,`` alisema. Alisema Ibara ya 17 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa fursa ya uhuru wa mwananchi kutoka sehemu moja ya nchi kwenda nyingine. Vilevile, Mwankenja alisema Ibara ya 13 (6) (b) (Presumption of Innocense), inasema mahakama pekee ndiyo yenye uwezo wa kumtia hatiani mshtakiwa hivyo kumyima ruhusa ya kusafiri ni sawa na kumhukumu kabla hajatiwa hatiani na mahakama. ``Justice must be done and seen to be done`` alisema Mwankenja akimaanisha kuwa haki lazima itendeke na ionekane dhahiri kuwa imetendeka. Hata hivyo, Mwankenja alisema Sheria za Bunge hazijaweka wazi kuhusu utaratibu mbunge anapopatwa na matatizo kama ya Mramba. Hakimu alisema Dodoma ni karibu hivyo ni rahisi kwa mshtakiwa huyo kusafiri mara moja na kufika Dar es Salaam endapo atahitajika, hivyo hakuna sababu yoyote ya kumzuia kusafiri. Alisema wadhamini wake lazima waarifiwe kuhusu ruhusa hiyo ya kusafiri ili wasiwe na hofu. Kesi ya Mramba na mwenzake Daniel Yona itatajwa tena tarehe 2 mwezi ujao. Mramba aliwasilisha ombi hilo kupitia wakili wake Herbert Nyange Januari 2 mwaka huu akitaka ruhusu ya kwenda jimboni kwake. Barua ya ombi hilo ilielekezwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo ikitaka ruhusa ya kuwa nje ya Jiji la Dar es Salaaam kuanzia Januari 3 mwaka huu hadi mwezi ujao. Mramba na Yona wanakabiliwa na makosa ya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuipatia mkataba wa kukagua uzalishaji wa dhahabu kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza na kampuni yake tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation, kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2002 na ile ya Madini ya mwaka 2002. Katika shitaka la pili, Mramba na Yona wanadaiwa kuwa Mei 28, mwaka 2005 wakiwa watumishi wa umma jijini Dar es Salaam, wakiitumikia serikali katika nafasi za uwaziri wa Fedha na Nishati na Madini, kwa pamoja walitumia vibaya madaraka yao kwa kusaini mikataba ya kuiongezea kampuni hiyo muda wa miaka miwili wa kuendelea kukagua madini ya dhahabu kuanzia Juni 2005 hadi Juni 2007 kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
SOURCE: Nipashe
Kipanya na busara zake ..

Saturday, January 3, 2009


UTAMU WATOWEKA MBEYA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupilia mbali rufaa ya mgombea wa Chadema kupinga kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mbeya Vijijini. Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala (pichani aliyenyanyua vidole vya ushindi)alienguliwa na Tume ya Uchaguzi ya Mbeya Vijijini baada ya vyama vya CCM na CUF kuwasilisha pingamizi, vikidai kuwa alikiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu.Mgombea huyo ambaye ni mwanasheria, hakukubaliana na uamuzi huo na kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Lakini leo, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mount Livingstone kuwa baada ya kutafakari mambo makuu manne, tume yake imetupilia mbali rufaa hiyo.

mgonja aunganishwa na akina mramba na yona



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, jana imemuunganisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Grey Mgonja, katika kesi ya watuhumiwa wengine wa ufisadi, Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona.

Wote hawa wanakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao na kulisababishia taifa hasara ya takribani bilioni 11.Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Hezron Mwankenja alifikia hatua hiyo kufuatia ombi la upande wa utetezi katika kesi ya Mgonja unaoongozwa na Profesa Leonard Shaidi, kuiomba mahakama hiyo kumuunganisha mteja wake na akina Mramba na Yona kwa kile alichodaiwa kuwa kesi hizo zinafanana.

Pichani aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba (kulia) akiteta jambo na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona (katikati) wakati walipokuwa mahakamani, mapema mchana hii leo Kushoto ni Grey Mgonja.

mmh mambo ya funga mwaka haya.!