Wednesday, April 28, 2010

KERO !!
Du kweli bongo tamu acha tu unajua kwa nini maana mambo yanavyo ahinishwa sivyo yanavyofanyika. Hii ilinikuta jana maeneo flani katika maswala ya kutaka kufanya huduma nao.
Sehemu hiyo ni ya kampuni moja maarufu sana hapa mjini. Natumai hili litakuwa tatizo la mfanyakazi wa kituo hicho. Kwa nini nasema hivi ? kwa sababu matumaini yangu ni kuwa wakubwa wanajitaidi hadi kuweka muda katika milango kama njia ya kuwadhibiti wafanyakazi wafunge kwa muda ulio ainishwa lakini wanasitisha huduma dakika ishirini kabla. Kwa maslai yao binafsi pasipo kujua wanapoteza wateja na kuwa ona ni watu wasioenda na muda.
Jamani huu ni uungwana ukikosa unasema nitapata lini na ukipata ndio unaanza kujipangia mambo yako unakiuka yale uliokubaliana nayo. Kutokana na hili kunapelekea wateja wapya na wazamani kuichukia huduma usika na kampuni kwa ujumla kwa ajili ya mtu mmoja. Jamani tujirekebishe na kibaya zaidi unakuta watu wanatetea kuwa muda umeisha na wakati kuna dakika kama ishirini za ziada kabla ya kufika muda ulio ainishwa na bango lao mlangoni ,
bongo bwana ukifanya mambo inavyotakiwa ndio unaonekana wakuja au mshamba . Alafu watu sie sie tuna sema hatuna maendeleo, o wageni wanachukua kazi zetu na kadhalika lazima wazichukue tu kama hatubadiliki tutaendelea kuongea wakati wenzetu ni vitendo tu .
Ni hayo tu
Kadidi hapa.
Pia unaweza acha comment katika kero hii.

No comments: