Wednesday, July 21, 2010

BREKING NYUUUUUZZZZZ: CHADEMA YAMTANGAZA RASMI DK. SLAA MGOMBEA WAKE WA URAIS LEO
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akitangaza rasmi leo kuwa Kamati Kuu ya Chama hicho imemteua Katibu Mkuu wao Dk. Wilbroad Slaa kuwa mgombea wao wa Urais katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano na wanahabari makao makuu ya chama huko Kinondoni jijini
waandishi na baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakimsikiliza Mh. Mbowe

Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe akitoa ufafanuziw a jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la MwanaHalisi Saeed Kubenea baada ya mkutano huo leo


MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MH. FREEMAN MBOWE LEO AMETANGAZA RASMI KWAMBA CHAMA HICHO KITAMSIMAMISHA KATIBU MKUU WAKE DK. WILBROAD SLAA KUGOMBEA KITI CHA URAIS KWENYE UCHAGUZI MKUU MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.

MH. MBOWE AMESEMA MCHANA HUU KWENYE MAKAO MAKUU YA CHADEMA YALIYOKO KINDONDONI JIJINI DAR KWAMBA KWA KAULI MOJA KAMATI KUU YA CHADEMA ILIYOMALIZA VIKAO VYAKE JANA IMEKUBALIANA KWA KAULI MOJA KUMUOMBA DK. SLAA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS, NA KWAMBA NAYE AMEKUBALI.

MBOWE AMEPANGUA HOJA KIBAO ZILIZOKUWA ZIKIPIGIA UKOPE UAMUZI WA CGHADEMA KUMPA DK. SLAA NAFASI HIYO AMBAYO MOJA KWA MOJA ATAKUWA HATETEI TENA KITI CHAKE CHA UBUNGE CHA KARATU, NA KWAMBA ENDAPO ATAKOSA URAIS ATAKUWA KAMALIZIKA KISIASA.

"OCTOBA 31 DK. SLAA ATAKUWA RAIS WA NCHI HII SASA UNAPOSEMA ATAKUWA AMEJIMALIZA KISIASA UNA MAANA GANI AMA NDIO UNAJIMU WENU AMBAO MMESHAUANZA.

"DK. SLAA NI MTU MAKINI NA MWENYE SIFA ZOTE ZA SIO TU KUWA RAIS BALI PIA KULETA MABADILIKO MAKUBWA AMBAYO NCHI HII INAYAHITAJI LAKINI HAKUNA WA KUTEKELEZA", ALISEMA MH. MBOWE KWA KUJIAMINI HUKU AKISHANGILIWA NA BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHRIA MKUTANO HUO NA WANAHABARI.

MWENYEKITI HUYO WA CHADEMA PIA AMEKANUSHA VIKALI UVUMI KWAMBA DK. SLAA AMETUMWA NA KANISA LA DINI FULANI KUGOMBEA HUO URAIS, NA KUDAI HUO NI UMBEA WA BAADHI YA MAGAZETI AMBAYO KADAI AIDHA WAANDISHI AMA WAMILIKI WANATUMIKA KUKIPAKA MATOPE CHADEMA.

"kUNA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINABAKA WANANCHI KWA KUANDIKA HABARI ZA UMBEA NA KUPOTOSHA KWA MANUFAA YAO (WAANDISHI BINAFSI) AMA WAMILIKI WA VYOMBO HIVYO.

"NAOMBA BAADHI YA WAANDISHI WENYE TABIA HIYO WAIACHE WASIJE WAKAIPELEKA NCHI PABAYA", ALISEMA MH. MBOWE HUKU MEZA KUU WALIYOKETI VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHADEMA AKIWEMO NAIBU KATIBU MKUU MH. ZITTO KABWE, WAKITIKISA VICHWA KUUNGANA NA KAULI ZAKE.

KUHUSU UBUNGE JIMBO LA KARATU ATALOACHA WAZI DK. SLAA MWENYEKITI WA CHADEMA KASEMA WAO HAWANA WASIWASI KWANI HAKUNA CHAMA CHENYE YBAVU WA KUTWAA KITI KATIKA JIMBO HILO AMBALO ALIONGEZEA KWAMBA HALMASHAURI YAKE YA WILAYA IMEKUWA IKONGOZWA NA CHADEMA KWA MIAKA 10 SASA.

"DK SLAA PAMOJA NA KUWA CHACHU KUBWA YA USHINDI WA CHADEMA KARATU LAKINI SI YEYE PEKEE MWENYE UMUHIMU MKUBWA KULE JIMBONI. KUNA VIONGOZI WENZIE NA WANANCHI AMBAO KWA PAMOJA NDIO WALIOIFANYA CHADEMA ISIMAME.

"HIVYO KAA UKIHJUA TAYARI KUNA MGOMBEA MAKINI AMESHAANDALIWA NA ATAFANYA MAKUBWA KAMA ALIYOFANYA DK. SLAA", ALIFAFANUA.

No comments: