Wednesday, August 12, 2009

mrisho mpoto aanzisha mjomba music band
msanii nguli wa mashairi mrisho mpoto ambaye ni maarufu kwa jina la 'mjomba'ameanzisha bendi itayoitwa jina hilo hilo - Mjomba music band. ameiambia globu ya jamii usiku huu wakati akitumbuiza kwenye ukumbi wa Nkrumah Hall chuo kikuu cha university of dar kwamba ana vijana 10 wa jinsia mbalimbali wanaounda kundi hilo lenye vionjo vyote vya muziki.
waimbaji wa mjomba music band wakiwa katika onesho lao la kwanza leo UDSM

muziki uliopokolea hakuna alieketi kitini
mjomba akishangiliwa kwa mambo yake mazito ya kuomba nauli waimba
tokomile, sindimba, bongo flava, sebene vyote unavipata Mjomba music band

mrisho mpoto akimtambulisha mwalimu wake wa shule ya msingi (shoto) na mjomba wake wa kwelikweli
mjomba music band katika picha ya pamoja

kwa mawasiliano na kundi hili piga namba
+255 754 987 838
au
+255 712 056 748
ama
mmpoto@yahoo.com



Tuesday, August 4, 2009

vijimambo vya nathan mpangala

TAARIFA YA IKULU KUHUSU SUALA LA KAMPUNI YA RICHMOND
Pichani ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Philemon Luhanjo na pembeni yake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maneno na vijembe ati kuwa kuna mkono wa Rais Jakaya Kikwete katika kutoa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopata Kampuni ya Richmond.
Kiini cha maneno hayo ni kauli za baadhi ya wanasiasa zilizopazwa sauti na baadhi ya vyombo vya habari.

Tunapenda kusema, tena kwa msisitizo, kuwa maneno hayo si ya kweli na hayana msingi wowote.
Rais hajahusika na uamuzi wa tenda hiyo kupewa kampuni ya Richmond kama vile ambavyo hakuhusika na kupewa tenda kwa kampuni za Aggreko na Alstom.

Kama mtakavyokumbuka wakati ule kampuni hizo tatu ndizo zilizopewa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura. Kampuni ya Aggreko ilipewa tenda ya kuzalisha umeme wa megawati 40 na Richmond kuzalisha megawati 105.6 pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Kampuni ya Alstom ilipewa tenda ya kuzalisha megawati 40 za umeme pale Mwanza kwa kutumia mafuta ya dizeli.

Katika uamuzi wa kupewa tenda kampuni hizo, Rais hakujihusisha, hakuhusishwa na wala hapakuwepo na sababu ya kuhusishwa au kujihusisha . Hiyo siyo kazi ya Rais. Hiyo ilikuwa ni kazi ya TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini na ndiyo walioifanya. Hayo ndiyo matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya Umma na ndivyo ilivyofanyika.

Katika shughuli nzima ya uteuzi kulikuwa na Kamati mbili za kushughulikia upatikanaji wa makampuni ya kutoa huduma ya mitambo ya kukodi ya kuzalisha umeme wa dharura. Ya kwanza ilikuwa Kamati ya Watalaamu kutoka TANESCO, Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini iliyokuwa na jukumu la kutathmini wazabuni wote waliojitokeza kuomba na kupendekeza wanaofaa kufikiriwa kupewa kazi hiyo.
Kamati ya Pili ilikuwa ni ile ya Serikali ya Majadiliano (Government Negotiating Team) iliyokuwa na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TANESCO, Benki Kuu na Shirikisho la wenye Viwanda kuwakilisha sekta binafsi. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kufanya majadiliano na wale waliopendekezwa na Timu ya Wataalamu na hatimaye kupendekeza anayefaa kupewa.

Kamati ya Majadiliano ilipomaliza kazi yake ilikabidhi taarifa yake Wizarani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ndugu Arthur Mwakapugi ambaye naye akaikabidhi kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Ibrahim Msabaha kwa uamuzi. Kama tulivyokwishasema mamlaka ya uamuzi yalikuwa chini yao. Hakuna wakati wowote katika mchakato wa kuamua kampuni ipi ipewe tenda alipofikishiwa Rais kwa uamuzi wake wala kutakiwa kutoa maoni.

Mambo aliyofanya Rais

Katika suala zima la kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme, Rais alihusika katika mambo manne. Kwanza, katika kuamua TANESCO itumie mitambo ya kukodi kuzalisha umeme na Serikali igharamie ukodishaji huo.




Suala hilo lilikuwa lazima liamuliwe na yeye kwa sababu lilikuwa linahitaji Serikali kugharamia ukodishaji. Kama si hivyo lisingefikishwa kwake kwani ni jambo ambalo lingekuwa juu ya TANESCO kuamua kukodisha na kulipia. Gharama hizo hazikuwa zimepangwa katika bajeti ya serikali hivyo ilikuwa ni lazima kupata idhini ya Rais ya kutafuta hizo pesa na kuzitumia kwa ajili hiyo.

Pili, Rais alihusika katika kuzungumza na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuwaomba wakubali sehemu ya pesa waliyopanga kuipa Tanzania kama msaada kutokana na mpango wa msamaha wa madeni itumike kugharamia ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme. Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond (ambayo baadae ikawa Dowans) na matumizi mengine ya dharura za umeme. Matumizi hayo mengine yalijumuisha pia ununuzi wa mitambo ya aina ya Watsilla ya kuzalisha megawati 100 za umeme pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Mitambo hiyo imeshanunuliwa, kufungwa na tayari inazalisha umeme.

Tatu, Rais alihusika katika vikao vya Baraza la Mawaziri vilivyojadili matatizo ya upungufu mkubwa wa umeme nchini na kuamua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo. Moja ya hatua zilizoamuliwa kuchukuliwa, ni hii ya kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme. Katika vikao hivyo vya Baraza la Mawaziri alitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika zoezi zima la kupata makampuni au watu watakaotoa huduma hiyo. Hususan, Rais alisisitiza kuwa pamoja na udharura uliokuwepo Kanuni na Sheria ya Ununuzi wa Umma zizingatiwe.

Nne, Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya USD 10 milioni na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane. Rais alikataa maombi yaliyopelekwa kwake na Wizara ya Nishati na Madini ya kumuomba aagize Wizara ya Fedha, iilipe kampuni hiyo fedha hizo. Rais aliagiza Wizara ya Fedha ibaki na msimamo wake na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wafanye mambo mawili. Kwanza, wafanye utafiti zaidi kujua undani wa Kampuni ya Richmond. Isije kuwa ni kampuni bandia wakapewa fedha wakatokomea nazo na mitambo isipatikane na hukuna namna ya kuipata kampuni wala wahusika wake. Pili aliagiza wawatake viongozi wa Kampuni ya Richmond kwanza walete mitambo, ikishafika, ndipo walipwe. Maagizo hayo ya Rais yalizingatiwa na Kampuni ya Richmond ikapewa sharti hilo. Lakini, ikashindwa kulitekeleza na kuishia kuingia mkataba na Kampuni ya Dowans iliyokuja kuleta hiyo mitambo badala yake.

Hivyo ndivyo alivyohusika Rais katika suala zima la ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kwa makampuni ya Aggreko, Alstom na Richmond. Kama kweli kungekuwa na mkono wake wa upendeleo kwa Kampuni ya Richmond kupata tenda, iweje tena yeye ndiye akatae kampuni hiyo isilipwe fedha za kianzio mpaka kuifanya ishindwe kazi? Ndiyo maana tunasema maneno hayo hayana msingi, yanasemwa na watu ambao ama hawaujui ukweli au wameamua kutokusema kweli kwa makusudi kwa sababu
wanazozijua wao. Tunatoa ufafanuzi huu kuwafanya Watanzania waelewe ukweli wa mambo.

Watumishi wa Umma

Kuhusu watumishi wa Umma waliohusika na uchambuzi wa zabuni, majadiliano na uamuzi, napenda kuwahakikishia kuwa, Serikali imelishughulikia jambo hili na sasa linafikia ukingoni.




Mamlaka za nidhamu zimeangalia mambo mawili: tuhuma za rushwa na uzembe. Tuhuma za rushwa hazijathibitika mpaka sasa na tuko tayari kuchunguza zaidi. Lakini tuhuma ya uzembe imethibitika kwa ukweli kwamba Kampuni ya Richmond haikufanyiwa uchunguzi wa kina kuijua kampuni hiyo kwa undani kabla ya kuipa tenda. Due diligence haikufanywa. Kwa sababu ya makosa hayo mamlaka za nidhamu husika kwa watumishi hao zitawachukulia hatua zipasazo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi.

Wenzetu hawa waliridhika tu na maelezo ya mwakilishi wa Kampuni ya Richmond aliyetosheleza masuala ya kuwa na mitambo ya kuweza kuzalisha megawati 105.6, mitambo ambayo itafaa kwa mfumo wetu wa umeme, itapatikana kwa wakati na umeme kuuzwa kwa bei nafuu. Ni kweli kwamba kampuni hiyo iliwashinda wazabuni wote kuhusu masharti hayo lakini walisahau msemo wa wahenga kuwa “si kila king’aacho ni dhahabu.” Naamini wangefanya uchunguzi wa kina kuhusu kampuni ya Richmond wangegundua kuwa ni ya bandia na haikuwa na uwezo wa kifedha wa kutekeleza zabuni ile. Kwa sababu ya upungufu huo hatua zipasazo za kinidhamu zitachukuliwa kwa kila mmoja kwa kiwango chake cha kuhusika.Yaani kwa uzito wa kosa lake. Kazi hiyo imeanza na inaendelea kufanyika.

Imetolewa 01 Agosti, 2009


PHILLEMON LUHANJO
IKULU,


KATIBU MKUU KIONGOZI


DAR ES SALAAM.
kiplefti yetu idumuuuuu, idumuuuuu....
ni wiki ya tatu sasa na kiplefti yetu iliyopo mtaa wa azikiwe street jijini dfar bado tu kufunguliwa rasmi. redio mbao zinadai (mh...u yale yaleeeee...) kwamba anasubiriwa mhandisi amalize likizo mwezi ujao mwisho aje atoa maelekezo nini kifanyike. waziri mkuu yupo tayari kukizindua kiplefti hichi wakati wowote kikiwa tayari.
katunisti nathan mpangala akiwa kwa watani wa jadi
katunisti nathan mpangala (mmatumbi) akiwa na animator wenzie toka ughaibuni kwenye mafunzo ya juu ya fani yao jijni nairobi majuzi
mojawapo ya mabango yaliyomvutia nathan kwa watani wa jadi

nathan akiwa na wamatumbi wenzie nairobi

moto kisiwani las palma wavunja safari ya FFU Hispania
The Ngoma Africa band
Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" juzi siku ijumaa 31.07.2009 walijikuta wakiishia uwanja wa ndege wa Bremen,huko Ujerumani baada ya idara ya usalama wa anga kutoruhusu ndege yeyote kuelekea katikia kisiwa cha "La Palmas" ambako bendi hiyo ilitegemewa kutumbuiza katika onyesho maalumu.

Kisiwa cha La Palma, kilichoko huko Hispania kimeshika moto na huduma zote za safiri wa ndege zimesimamishwa, na zimesababisha pia kutosafiri kwa bendi hiyo maarafu "The Ngoma Africa" aka FFU.

Ilikuwa wasafiri kwa ndege maalumu ya kukodi wamejikuta wapo uwanjani na HAKUNA SAFARI.

bendi hiyo ndiyo inayoongoza kwa kukamua na kuwatia kiwewe washabiki

bofya chini kusoma jarida la africa news uone mambozzzz.

entertainment/the-ngoma-africa-band-
continues-to-thrill-fans.html

Monday, August 3, 2009

ama kweli pombe si juisi





Kuna picha hizi za kuvunja mbavu za walevi tungependa tushee na wadau waburudike
Picha zaidi unaweza ukawapa wadau link hii

http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=129431
NIFAHAMISHE.COM TEAM

heka heka za kabla ya kuwasili kwa mwenge wa uhuru

Vijana wakifurahia kuwasili kwa menge wa uhuru
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Jordan Lugimbana akipita kuwasalimia viongozi mbalimbali
Maelekezo ya awali yalikuwa yakitolewa kabla ya Mwenge wa Uhuru kuwasili uwanja hapo.
Walikuwepo vijana mbalimbali kutoka mataifa ya nje ambao pia walifika kuupokea Mwenge wa Uhuru.

Ilikuwa ni furaha tu wanjani hapo
Vijana wakifurahia kwa mapokezi ya mwenge wa uhuru
Watu mbalimbali wakicheza na kuimba huku wakisubiri kuwasili kwa menge wa uhuru uwanjani hapo.
Wajasiliamali pia hawakukosa viwanjani hapo
Vijana kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiimba nyimbo mbalimbali kuhusiana na Mwenge wa Uhuru uliowasiri jana jioni Kata ya Kawe katika viwanja vya Tanganyika Peka,Kinondoni jijini Dar.Mapokezi ya Mwenge huo yalikwenda sambamba na uhamasishaji wa mbinu mbalimbali za kupambana na ugonjwa wa UKIMWI ikiwemo na kupima afya kwa hiyari.
Pichani ni bendera za mataifa wakilishi mbalimbali zikiwa zinapepea
Mbio za Mwenge wa uhuru zilikuwa kata ya Kawe jana jioni katika viwanja vya Tanganyika Pekaz,ambapo watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali walihudhuria mapokezi ya mwenge huo wa Uhuru uliokuwa umebeba kauli mbiu ya "pinga unyanyasasi wa jinsia,watoto na mauaji ya albino".Mwenge huo ulipokelewa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Jordan Lugimbana.

Wednesday, July 29, 2009

Toyota Pickup for Sale




TOYOTA PICKUP HILUX
YEAR 2003
PETROL
PRICE 16 MIL. FIXED!!
CONTACTS 0754 337957
0715 336063
DAWASCO MAMBO MSWANO
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom Ephraim Mafuru akizungumzia huduma ya kulipia maji kwa kutumia huduma ya simu ya mkononi M-Pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ofisi za Dawasco jana.waliokaa katika ni Mkurugenzi wa biashara wa Dawasco Raymond Mndolwa na Meneja habari wa DAWASCO Shabani Salum.

WATEJA WA DAWASCO SASA KUWEZA
KULIPA BILI ZAO KUPITIA VODAFONE M-PESA

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa mara nyingine imewawezesha wateja wake kulipa bili za maji kupitia Vodafone M-Pesa.Kwa sasa wateja wa vodacom wamewezakulipa bili zao za maji kwa kila mwezi kupitia Vodafone M-Pesa.Ni siku chache tu tangu kutangazwa kwa malipo ya LUKU kupitia Vodafone M-Pesa.

Mkurugenzi Masoko wa vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema katika makao makuu ya DAWASCO, kuwa kwa niaba ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Tungependa kuwakaribisha DAWASCO katika ulimwengu wa Vodafone M-Pesa. Vodafone M-Pesa ilianzishwa mapema mwaka jana(2008) kama huduma ya kusafirishia pesa kutoka kwa mtu mmoja kuelekea kwa mwingine.Huduma hii imeendelea kukua na kupanuka hadi kuwawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili,ada za shule na ulipaji wa mikopo.

Vodafone M-Pesa ni njia rahisi ya kutuma hela kwa kutumia simu za mkononi.Mtandao huu wa Vodacom M-Pesa uliyowawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili zao za maji DAWASCO.

Mafanikio ya huduma hii yamefanikiwa kwa ushirikiano baina ya Vodacom Tanzania na DAWASCO.Kwa Kampuni hii ya simu za mikononi ya Vodacom tunajua huu ni mwanzo tu, Bado tutaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika mengine katika kukuza na kutoa huduma hii kwa ubora zaidi kwa wateja wetu.alisema Mafuru

Akiongelea huduma hiyo Afisa biashara wa DAWASCO Raymond Mndolwa amesema, Sisi kama DAWASCO tutaendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu kupitia mitandao tofauti ya mawasiliano.

Tunatumai wateja wetu watafurahia kutumia huduma hii ya kulipa bili ambayo itarahisisha maisha Yao.

DAWASCO imeahidi uboreshaji
zaidi katika huduma zao