Thursday, February 19, 2009

Ya Kale Dhahabu: Pijoti La Urithi Hili !
Peugeot 203. Liko Makanyagio, Iringa. Tunaambiwa Ulaya na Marekani kuna watu wenye kupanda madau kwa vitu kama hivi.

Davidson Kiwia na Vivian
Wanameremeta..

Mdau Davidson Kiwia kaachana na Club ya Ukapera na Kufunga pingu za Maisha na Kimwana Viviana Massawe kanisa la Kilutheri la Azania Front Jijini Dar es Salaam na kufwatia na sherehe la nguvu.kwa wadau mbalimbali mtakaopenda kudungwa picha za maaana kwenye harusi kama hizi wasiliana na Mdau Abdallah Mrisho kwa simu number 0713 839363 au Email:abbymrisho@gmail.com
Hivi Mheshimiwa
Slaa..
Ni

Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Laurance Masha(Kushoto)akitete jambo na Mbunge wa Karatu Mheshimiwa Dr Willbroad Slaa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Wednesday, February 18, 2009





MWANAMUZIKI mahiri wa Msondo Ngoma, Joseph Maina amefariki ghafla jana asubuhi akiwa ndani ya daladala.
Dereva wa basi la daladala lenye namba za usajili T582 AFL linalofanyika safari kati ya Mwenge na Temeke Mikoroshoni, Kassim Salum aliiambia Mwananchi jana kwenye Hospitali ya Temeke kuwa msanii huyo alifariki akiwa amekaa kiti cha mbele mlangoni.
"Unajua aliwahi kuingia, na sisi ilikuwa zamu yetu kupakia hapo Temeke Mikoroshoni, kulikuwa na abiria anataka kupanda, nilipomwambia asogee kiti cha kati, nikaona anakakamaa na muda mfupi akalala.
"Baada ya kuona hali ile, watu walijaa na niligeuza gari hadi kituo cha polisi Maghorofani, lakini na wao walinipa askari wakaniambia tuelekee hospitali ya Temeke," alisema Salum.
Hata hivyo, mwili wa Maina ulibakia kwenye kiti cha daladala kwa takriban saa nzima katika hospitali hiyo huku mashabiki na watu wengine wakielezea kumfahamu kama ni Maina. Mwananchi ilifika hospitalini hapo na kukuta umati wa watu wakielezea masikitiko yao kutokana na kifo hicho.
Saa 7:11 mchana, kiongozi wa Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo aliiwasili akifuatana na mpiga solo, Said Mabera, wacheza shoo na wanamuziki wengine.
Hata hivyo, wasimamizi wa chumba cha maiti walimruhusu Mabera kwenda kutambua mwili na aliporudi alithibitisha kuwa kweli ni Maina.
Gurumo alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na miguu na bendi walikuwa wakiandaa utaratibu wa kumtafutia matibabu.
"Kwa kweli ni pigo kubwa kwani Maina alishiriki katika nyimbo zote za Msondo, alishiriki albamu zote ni pigo kwa sasa hatuna la kusema tutatoa taarifa," alisema.
Maina ambaye ameacha mke na watoto wa wawili alitunga kibao kumuimbia mke wake, Mama Cossy ambacho hakijatoka.
Maina ameongeza pengo la wanamuziki wakali wa bendi hiyo waliofariki miaka ya karibuni, akiwemo TX Moshi William, Athumani Momba na Suleiman Mbwembwe.

NATIONAL STADIUM

Huu ndio lunyasi ndani ya Uwanja wa taifa baada ya kukamilishwa kwa zuria la kukimbilia wambulu na kukabidhiwa juzi na wachina kwa wabongo waweze kufanya mambo! Ila kweli tukiachia mameneja kama waliopo sasa hivi tutafika kweli?

Kibonzo cha leo !!!!

MNASHANGAA?

Jamani muda mrefu mzee Mkapa alikuwa hajaonekana mitaani, hata Sumaye lakini kikubwa alichotuachia ni uwanja mpya wa taifa kumbe hata yeye alikuwa hajauona? Cheki anavyoshangaa!!! Watanzania badala wamwache mzee wa watu ale uzee vyema wanamletea fitna!

Monday, February 16, 2009

MATUMLA ABONDWA

Nyumbani ni nyumbani tu, Cheka akipongezwa na walugulu.
Afande Sele akimpongeza Cheka baada ya Ushindi, hii ni mambo ya Dar mpaka Moro.

Mashambulizi yakiendelea usoni mwa Matumla.


Matumla akiondoka akiwa hoi baada ya kichapo hasa round ya 11 kidogo aanguke.
RC Moro, Said Kalembo akimvika mkanda wa Ushindi Cheka.

BONDIA francis Cheka jana usiku aliendeleza ubabe wake kwenye familia ya Matumla baada ya kumpiga kwa mara ya tatu Rashid Matumla kwa pointi kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania ulishudia mabondia hao wakionyesha ujuzi wa kutumia makonde katika raundi zote 12 za mchezo huo.
Majaji wote watatu walimpa Cheka ushindi wa pointi 19/18 dhidi Matumla aliyeonyesha upinzani mkali kwa bingwa huo wa ICT.
Rashid Matumla kabla ya mpambano huo alisema endapo atapigwa atatangaza kujiuzuru rasmi. SIJUI INAKUWAJE SASA?

SANGOMA KUKIONA MZA




Waganga waanza kufanyiziwa kuokoa maalbino
AGIZO la Waziri Mkuu alilotoa wakati wa ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa kuhusiana na ukomeshaji wa mauaji ya albino, limeanza kutekelezwa baada ya vibanda 17 vya nyasi mali ya waganga wa jadi kubomolewa wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Zoezi hilo la ubomoaji ambalo limefanyika kwa mgambo wa jiji la Mwanza katika zoezi lililosimamiwa na viongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza chini ya mkurugenzi wake Willson Kabwe.
Vibanda vya nyasi vilivyobomolewa ni 13 pamoja na nyumba nne za nyasi ambazo ni mali ya mganga Masai Kasanga aliyekuwa amejenga jirani na shule ya sekondari ya Lumala iliyopo wilayani Ilemela jijini Mwanza. Akielezea zoezi hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Willson Kabwe, alisema mamlaka yake imeamua kutekeleza agizo hilo la serikali ambalo lilitolewa na maelekezo yaliyotolea na mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. James Msekela katika hotuba yake wakati wa kupokea maandamano ya maalbino jijini Mwanza.
“Zoezi la leo ni utekelezaji wa agizo la serikali, na hili litakuwa ni zoezi la kudumu kwa vile ujengaji wa vibanda hivi unapingana na sheria ya mipango miji ambayo inazuia kuwepo kwa vibanda katika maeneo ya taasisi ama makazi ya watu. Litakuwa endelevu na leo tumeanzia hapa Ilemela”Alisema Kabwe.
Alisema kabala ya kumvunjia mganga huyu alipewa taarifa ya kuhama na kubomoa vibanda vyake ikiwa ni pamoja na kulipwa fidia ya ardhi ya eneo hilo sh. 1.2 milioni ambalo alikuwa akilimiliki kihalali lakini licha ya kupokea fidia hiyo aligoma kuhama hatua ambayo imelifanya jiji kuchukua hatua hiyo.
Akielezea hatua hiyo mganga huyo Masai Kasanga ambaye ni mwenyeji wa Bukumbi wilayani Misungwi alisema hakuweza kuhama licha ya kutakiwa kufanya hivyo na kulipwa fidia kutokana na ukweli kuwa fidia hiyo ni ndogo na kwamba uongozi wa jiji haukumpa fidia ya kuhamisha mali zake pamoja na wagonjwa wake.
“Nilipokea fidia lakini niliwaeleza kuwa wanapaswa kunipatia na fedha ya kuhamisha wagonjwa wangu pamoja na vitu vyangu hawakunipa ndiyo maana sikuhama, lakini sasa wamefanya hivi, basi” alieleza.

DOGO AULA KWA PINDA




Mtoto George Bush wa Chato ambaye amechukuliwa na familia ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa ajili ya kumlea maisha yake yote mpaka atakapojitegemea! Dogo ameahsanza kutanua na mzee katika ziara! Big Up Mzee Pinda, Upendo wa hali ya juu!