Hacker Geohot Aajiriwa na Facebook
Geohot,
hacker maarufu aliyejailbrake iPhone ameajiriwa rasmi na Mark
Zuckerburg, yaani Facebook. Hacker huyu ambaye pia aliwahi kushitakiwa
na Sony kwa shughuli za uchakachuaji baada ya kuihack PS3 na kuruhusu
watumiaji kuweza kutumia DVD feki za kuchakachua. Facebook
hawakuthubitisha Geohot atafanya kazi gani kwenye kampuni hiyo. Hacker
huyu ambaye anatumia majina mbali mbali katika shughuli zake pevu ikiwa
ni pamoja na million75, mil, dream na hax0r ameshafanya fujo nyingi sana
katika ulimwengu wa kompyuta. Kijana huyu kwa sasa ana umri wa miaka 22
tu.
Jina
alilopewa na wazazi wake ni George Francis Hotz. Katika kazi za
karibuni kabisa alizofanya hacker huyu ni kujailbraik iPhone na iPod
Touch kwa kutumia njia aliyoiita Blackra1n na pia kuifungua (sim unlock)
simu hiyo kwa njia aliyooiita blacksn0w.
Alipoihack
PS3 Sony walimpandisha kizimbani, hata hivyo mwezi wa nne mwaka huu
Sony na Geohot walikubaliana nje ya mahakama na hivyo Sony kufuta kesi
ile. Geohot alipewa sharti la kuto-hack tena PS3 ili kufutiwa kesi hiyo,
sharti ambalo alilikubali. Ajira hii kwa dogo huyu ni hasara kubwa kwa
wachakachuaji kwani watakosa mengi pale atakapotingwa na kazi za
Facebook. Hacker huyu huwa hana noma, baada ya kufanya mambo yake
huyaweka wazi kabisa katika tovuti yake ambayo ni www.geohot.com
Kwa sasa kwenye tovuti yake ameacha ujumbe mfupi wa ajabu, waweza kwenda kuangalia mwenyewe.
No comments:
Post a Comment