Utafuta kila kitu kwa kubonyeza “Delete” halafu kwenda jalalani(Recycle bin) kufuta kila kitu? Au utaamua kuformat na kuifanya kompyuta yako kufuta kila kitu?
Majibu ni mengi na inategemea na ufahamu wa muhusika,ila ukweli ni kuwa kwa njia zote mbili za hapo juu hakuna hata njia moja iliyo salama,kwani kama utatumia njia kama hizo na ukamuuzia
mtu mwenye utaalam wa kompyuta,basi ataweza kuzirudisha(recover) kumbukumbu zote ambazo mwenyewe ilizani zimefutika.
Jinsi gani kompyuta inahifadhi kumbukumbu?
Wengi wetu wanaweza wakawa wameshaanza kujiuliza,inakuwaje sio salama wakati nimeshafuta kila kitu toka kwenye kompyuta? Je mtu ataweza vipi kuona mafaili ambayo tayari nimeshayafuta?
Ukweli ni kuwa,kwa mujibu wa uhifadhi wa kumbukumbu kwenye kompyuta.Pindi unapofuta au kufanya format(kuweka mtambo endeshi(OS) mpya),sio kweli unayafuta moja kwa moja mafaili na kumbukumbu
toka kwenye kompyuta yako.Kitu kinachofanyika ni kuwa unaondoa taswira yake kwenye uso wa mbele wa hard disk hivyo kukufanya wewe uone kama umeyafuta ila bado yanaendelea kuwepo kwenye disk yako.Na hii ndio maana kama kunatokea kesi,wataalam wa uchunguzi wa makosa ya kompyuta(Computer Forensic) huchukua kompyuta yako kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi.
Siku hizi kuna program nyingi sana ambazo zina uwezo wa kurudisha mafaili hata yale yaliyokuwepo kipindi ulipoinunua kompyuta kwa siku ya kwanza, mara nyingi jinsi gani unaweza kuyarudisha
hayo mafaili hutegemea elimu ya mtu anayefanya hizo kazi ya kuyarudisha,kwani kazi ya kuyarudisha haya mafaili huwa ngumu kutegemeana na jinsi mafaili hayo yalivyofutwa.Mfano faili
lililofutwa kwa kubonyeza “Delete” ni rahisi zaidi kulirudisha kuliko lile lililofutwa kwa kuformat kopyuta, vilevile huwa ngumu zaidi kama mtumiajai alifanya mgawanyo wa hard disk (partition) baada ya kuformat.
Hivyo leo hii nitakuonehsha njia thabiti za kufuta kumbukumbu toka kwenye kompyuta unayotaka kuiuza ili kuhakikisha unakuwa salama zaidi.
Nitafutaje kumbukumbu moja kwa moja toka kwenye kompyuta ?
Takwimu z inaonesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne wamekuwa wakiibiwa siri zao kutokana na kuuza kompyuta bila kufuta kumbukumbu,hivyo kama wewe hutaki kuingia kwenye hilo kundi basi unaweza kufuata hatua zifuatazo.
1.Chukua ile CD uliyopewa pindi uliponunua kompyuta yako,ambapo nyingi huitwa recovery CD.Kama umepoteza hii CD au haukupewa pindi uliponunua kompyuta,basi nenda online na tafuta programu z inazotumika kufuta kumbukumbu(disk-wiping program). Programu hizi zipo nyingi ila binafsi nimewahi kutumia Darik’s Boot and Nuke (DBAN) hivyo nakushauri uijaribu hii.
2. Tumia programu kama Nero au yoyote uliyoizoea kuchoma hayo mafaili ya hii programu kwenye CD,kumbuka kuchagua mtindo wa Bootable CD.
3.Weka CD kwenye kompyuta yako halafu irestart. Kompyuta inatakiwa kuitambua hiyo CD pindi tu inapowaka,kutatokea ujumbe kwenye kioo unaosomeka “press any key to boot from CD.” Hapo bonyeza kitu chochote kwenye keyboard yako.
Kumbuka: Kama hautouona huu ujumbe unaosomeka”boot from CD” inawezekanika kabisa umekosea katika kuchoma hiyo CD yako,unatakiwa kuichoka kama “Bootable CD”.
Jaribu tena au wasiliana na mtaalamu wa IT aliye karibu nawe. Kama una uhakika kabisa uliichoma kama Bootable CD,basi inawezekana kuna mabadiliko unatakiwa kuyafanya ili kuiwezesha kompyuta kuitambua CD,haya kwa wasio na utaalam inabidi wawatafute wenye utaalam kidogo ili wakusaidie kubadilisha utaratibu wa BIOS.
Kama unataka kujaribu mwenyewe,basi kompyuta inapowaka tu bonyeza “Delete”,baada ya hapo fuata maelekezo na kuingia kwenye “Boot Sequence”,iweke CD or DVD kuwa ya juu kabisa kabla ya Hard drive,hapo mambo yatakuwa sawia.
4. Fuata maelekezo utakayopewa na hiyo programu,mara nyingi huchukua masaa kadhaa hadi siku mpaka kufuta kila kitu kilichopo kwenye kompyuta yako.
Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.
Baada ya hapo basi kompyuta yako itakuwa mbichi kabisa na unaweza kuiuza bila utata wala hofu juu ya kumbukumbuku wala usalama wako.