Friday, November 19, 2010

TEKNOLOJIA MPYA YA UJENZI KUPUNGUZA
UHABA WA NYUMBA TANZANIA

Pichani ni ujenzi wa mfano wa nyumba hizo

Tatizo sugu la ukosevu wa makazi hivi karibuni litapata ufumbuzi nchini Tanzania. Ufumbuzi huu upo karibu sana tofauti na wanavyofikiria watu wengi. Pale Wazo Hill, tarehe 18 Novemba 2010, wadau wa masuala ya ujenzi walishuhudia utengenezaji wa technolojia ya Moladi foamwork ambapo nyumba iliyotengenezwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa kutumia njia nafuu zaidi ambayo hivi karibuni inatarajia kuingia soko la nchini.

Uhaba wa upatikanaji wa makao nchini kwa ajili ya wale waliopo mijini kumeleta ongezeko za nyumba zinazojengwa kiholela. Kumekuwepo na ongezeko la mahitaji ya nyumba na hivi kusababisha uhaba na uhaba huu umekuwa ukiongezeka kila mara. Inakadiriwa kuwa upungufu wa makazi kwenye miji ya Tanzania inafikia nyumba 1.2 milioni.

Moladi Tanzania, ambao ndio wakala pekee wa teknolojia ya Moladi imedhamiria kutoa ufumbuzi wa uhaba wa makazi kwa kutengeneza nyumba kwa kutumia muda mfupi kwa kutumia Moladi formwork. Urahisi na kasi ya teknolojia ya Moladi imerahisisha ujenzi na kwa mafanikio kwenye baadhi za nchi za Afrika kama Zambia, Ghana, Zimbabwe, Angola, Botswana, Mozambique, Nigeria na Afrika Kusini.

Tangu mwaka wa 1986 Moladi imeleta njia mbadala tofauti na ujenzi uliozoeleka na inakidhi unafuu, ubora na uimara. Moladi foamwork ni ya kipekee, nyepesi, inaweza kurudiwa kwa matumizi mengine na yenye gharama nafuu.

Nchi yetu ambayo haina muundo mbinu ya uhakika, Moladi inaleta ufumbuzi ya makazi nafuu yanayoleta maendeleo katika jamii. Teknolojia ya Moladi na uimara wake inapunguza gharama na kuleta makazi imara na madhubuti ambayo inajengwa kwa muda mfupi sana.

Kampuni ya ukandarasi ya Holtan (E.A) ndio kampuni teule nchini Tanzania kwa ujenzi wa Moladi nchini ambapo wanauwezo wa kujenga nyumba nyingi kwa muda mfupi ambayo ni imara na yenye gharama nafuu.

Ushirikiano wa Holtan na Moladi inatokana na kiu ya kukidhi mahitaji ya makazi kwa kutumia mbinu ziliyozoeleka na teknolojia ya Moladi ambayo itachangia maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

Kuonyeshwa kwa umma kwa mradi huu wa Moladi tarehe 18 Novemba ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuifanya Tanzania kuwa ya kwanza kuutumia teknolojia ya kuongeza makazi ya Moladi.

Kwa maelezo zaidi kuhus Moladi Tanzania wasiliana nao kwenye namba ya simu: +255222701588/90
au barua pepe

No comments: