Monday, September 7, 2009

Yesu Mpya Aibuka nchini Urusi, Ana Maelfu ya Wafuasi

Kaka kadidi,Kuna habari hii tungependa

tushee na wadau wa blogu ya Inawezekana.
===================================
Yesu Mpya Aibuka nchini Urusi,
Ana Maelfu ya Wafuasi

Jamaa mmoja wa nchini Urusi amejitangaza kuwa yeye ni Yesu mtoto wa Mungu na amejipatia wafuasi wengi sana nchini humo wanaoamini kuwa yeye kweli ni Yesu.
Akifuga madevu na nywele ndefu, Yesu wa Urusi huzungukwa na wafuasi wake kila anapoenda na amefanikiwa kujikusanyia wafuasi wengi nchini humo na baadhi ya nchi za ulaya.
Yesu huyo mpya anayeitwa Sergei Torop mwenye umri wa miaka 48, awali alikuwa akifanya kazi kama trafiki polisi kabla ya kuachishwa kazi na baadae kudai kuwa mungu amemtuma kuwaokoa watu.
Torop amefanikiwa kujikusanyia wafuasi wengi zaidi ya 5,000 wakiwemo wasomi wakubwa nchini Urusi, wasanii na baadhi ya wanasiasa ambao humiminika kwenye kijiji chake cha Petropavlovka kilichopo maili 200 kutoka mji mkuu wa Urusi Moscow kwa nia ya kumuabudu.
Si ajabu ukipita kwenye kijiji hicho na kukuta watu wamepiga magoti mbele ya picha yake wakisali.
kwa habari kamili link ni hii:
http://www.nifahamishe.com/
NewsDetails.aspx?NewsId=2981654&&Cat=2
============================================
Thanks

Nifahamishe.com

No comments: