Saturday, September 26, 2009

dereva anaposusa kuendesha gari lililoshona

Kaka Kadidi2!
Basi bwana siku ya Idd ili kuwa taabu kidogo ya usafari hapa London. Nilipanda bus hili maeneo ya East Ham kuelekea Walthamstow, na tulivyofika mitaa green street abiria kibao wakapanda. Dereva akanuna na kususa kuendesha Bus eti sababu ya health and safety risk. Ebo fikiria hapo ingekuwa Kibongo- bongo ingelikuwaje. Ajabu na kweli ni kwamba hadi naondoka abiria ambao wengi wao walikuwa ni wa asili ya Asia walikataa katakata kuteremka. Sijui kwa bongo mambi yangekuwaje hapo??

Mdau Diaspora writer

No comments: