Wednesday, September 23, 2009

wadau kama kawa mie mjumbe tu wa SERIKALI YA UBUNGO MATAA.!

Nilikuwa kwenye kituo cha basi ( standi ya mkoa ) asubuhi nikasimamisha taxi ambayo ilikuwa inatokea ubungo kwenda shekilango , nilipoingia ndani ya gari mara vijana 2 wakaja , mmoja akaaa nyuma ya gari yule wa mbele akamfuata dereva akamlazimisha ampe shilingi 500 za kupakia , dereva akabishana nae lakini mwisho akampa,tulienda na gari mpaka magomeni ndio dereva akashituka tairi la nyuma moja halina upepo .
Wakati anabishana na wale vijana mmoja alaingiza spoku kwenye tairi moja ya gari kama adhabu yake ya kubishana wakati wa kutoa pesa , kama wasipofanikiwa kutoa upepo basi kiongozi wao mmoja anaweza kuja kumchapa makofi dereva , pamoja na unyanyasaji mwingine .
Hapo hapo wale wanaopanda dala dala wanajua vituko wanavyokutana navyo kama vijana wengine wanaokaa kituoni hapo zaidi ya masaa 2 kusubiri gari wanapopata hilo gari anaweza kwenda kushuka kituo kinachofuatia zaidi wanapenda kushuka mahakama ya ndizi au manzese tiptop , wakishafanya hivyo ujue ndani ya ya gari lazima kuna mtu atakuwa kaibiwa mali yake .
Kuanzia Asubuhi na mapema kuna kuwa na wafanyabiashara mbali mbali eneo la ubungo mataa , muda wa asubuhi wengi wa wafanya biashara ni wale wa magazeti na vifaa vidogo vya magari ambavyo ni rahisi kubebeka pindi askari wa jiji wanapovamia eneo hilo , kuna wengine wanaouza vocha za simu , kuna matapeli na kila aina ya wafanyakazi .
Wale wote wanaofanya kazi za kuuza magazeti wenye vibanda vyao , wale wanaotembeza njiani , hutakiwa kulipa karo Fulani , sio kwa serikali bali ni kwa watu wengine ambao wachukua wajibu huo wa kukusanya hayo mapato bila ridhaa ya serikali , mfano mwenye kibanda cha magazeti huwa analipa kuanzia 500 mpaka 800 kwa siku .
Madereva wa taxi ambao hupaki magari yao karibu na eneo hilo nao hutakiwa kulipa karo kwa siku , vile vile hao wanaochukuwa makato hao ni wababe wa maeneo hayo ambao wakishafanya uhalifu huo wanaenda kujificha katika mto ambao uko karibu na njia panda ya chuo au nyumba za karibu na mataa .
Vijana pamoja na madereva wakikataa kutoa hizo pesa ni kupigwa , wanapopeleka malalamiko yao kituo cha karibu yaani ubungo standi , wahalifu hawa huwa wanakamatwa na kuachiwa baada ya dakika chake na tatizo huja kwa Yule ambaye alimpeleka mhalifu kutuo cha polisi atakuwa hana amani na eneo hilo tena ni kupigwa na kufanyiwa visa vingine .
Kundi hili la vijana linaongozwa na watu 2 mmoja anaitwa Hemedi pamoja Tembo , hemedi ni mwenyeji wa maeneo hayo ya mataa inasemekana baba yake ana nyumba eneo hilo , na yeye ndio kiongozi wa kuendesha vipigo kwa wale ambao hawalipi hizi pesa .Kama nilivyosema huko juu hawa wanaopigwa na kulipishwa pesa hawadiriki kwenda tena kutuo cha polisi kwa sababu ya usalama wao , basi pale pale kituoni kuna maaskari ambao wanapokuwa na njaa huenda kwa vijana wengine ambao kazi yao ni kuuza vipande vya sabuni vilivyo mfano wa simu .
Hawa askari kanzu wanajua kabisa sasa hivi Fulani ameshauza simu nae anaenda kupata mgao wake , na ndio hawa hawa unapouziwa simu bandia unapeleka kesi kwao .Biashara ya simu za sabuni mara nyingi zinakuwa na watu zaidi ya 3 , kuna mmoja ndio mwenye simu halali na ndio mmiliki wa simu , huyo ukimwona ni mtanashati amependeza anaishi mjini kwa shuguli hizo kukodisha simu yake kwa hawa vijana , halafu kuna wengine kazi yao kuangalia kama kuna yeyote anayewaona wanaitwa site mirror , halafu kuna Yule ambaye ndio ameshika simu bandia ni watu wenye uelewano mkubwa sana .
Kama wamekuuzia ukafanikiwa kuondoka ukashituka mbeleni bahati yako mbaya au nzuri ila kama wamekuuzia ukawapa hela ukashituka pale pale manaa yake unaweza kugeuziwa kibao wewe , ukapigwa na kuitwa mwizi , unaweza hata kuchomwa moto .
Hii ndio serikali mpya ya ubungo mataa – wahusika wachukue hatua dhidi ya makundi haya yanayozidi kuchipuka kila mara

No comments: