Saturday, September 26, 2009

TBL yaipiga jeki kamati ya usalama barabarani
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu akibandika stika kwenye gari Dar yenye maneno yanayotahadharisha madereva kutoendesha magari huku wakiwa wamelewa. Stika hiyo ni moja kati ya 4000 zilzotolewa msaada na TBL kwa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Jana. Pia TBL ilitoa msaada wa fulana 800 kwa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe,
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 800, Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe, ikiwa ni msaada kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayoadhimishwa mkoani Mbeya kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 3, Mwaka huu. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar jana, TBL walikabidhi pia msaada wa stika 4000, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.


No comments: